Muhubiri Maarufu Nchini Marekani Afariki Akiwa na Miaka 99

Muhubiri Maarufu Nchini Marekani Afariki Akiwa na Miaka 99
Mhubiri maarufu nchini Marekani na duniani, Billy Graham amefariki duniani akiwa na umri wa miaka 99.

Graham ambaye ni raia wa Marekani aliyeanza kuhubiri jijini London Uingereza mwaka 1954, alikusanya maelfu ya watu kila mahali alipofanya mikutano ya injili.

Katika eneo la Afrika Mashariki, Graham aliwahi kuhubiri Tanzania miaka 55 iliyopita, wakati ikiitwa Tanganyika ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya Afrika aliyoifanya katika miaka ya 1960.

Inaelezwa kuwa katika mkutano wake uliofanyika Februari 28,1960 watu 40,000 walihudhuria mkutano wa siku moja.

Hata hivyo, taarifa iliyopatikana katika mtandao wa shirika lake haikueleza ni sehemu ipi mkutano huo ulifanyika mbali ya kufahamisha makadirio ya watu waliohudhuria.

Mhubiri huyo ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa viongozi wabaguzi wa rangi amehubiri zaidi ya watu milioni 210.

Graham, akiwa na umri wa miaka 16 baada ya kumsikiliza mhubiri mmoja alianza huduma ya mahubiri mwaka 1939.

Mhubiri huyo alifanya kazi kama ofisa wa mauzo na aliendelea na kuwa mmoja wa wahubiri wenye ushawishi mkubwa miongoni mwa watu wa dini zote huku akiwashauri marais na viongozi wengine wengi duniani juu ya imani ya Kikristo.

Mwaka 1949, alipata umaarufu wakati akihubiri kwa wiki nane kwenye hema kubwa huko Los Angeles. Graham ni mhubiri aliyeepuka kashfa mbalimbali zilizowazonga wahubiri wengi waliotumia vituo vya televisheni kusambaza injili.

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nasikia wala hakuwa na haya mahubiri au mafundisho ya siku hizi ya toa hela ili upatiwe huduma ya kiroho. Kwani biblia yasema umepewa bure toa bure. Siku hizi hata mtumishi akisema nimekuombea basi ujue kasema nakudai. Nawasihi watu wote, tafadhali jiepushe na yeyote, hata km ana jina kubwa kiasi gani na hata km anaombea wafu na wakafufuka, kamwe usipoteze senti hata tano. Kwani haruhusiwi kuuza maombi au individual. Ni siku za mwisho hizi. Biblia yasema watu watapenda pesa.jihadhali,wapo wengine hata wanauza maji, juice ya black currants na mafuta ya zeituni, olive oil, na Nasikia wengine hata wametajirika kupitia hilo. Mwenye nia ya kumjua Yesu, tafadhali chukua muda uisome Bible wewe mwenyewe. La sivyo wajanja watakudanganya.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad