Mzee Mwinyi Afuta Kauli yake Iliyodumu kwa Miaka 30

Mzee Mwinyi Afuta Kauli yake Iliyodumu kwa Miaka 30
Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi amekiri kufuta kauli yake iliyodumu kwa takribani miaka 30 kuwa Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu na haitakaa ifanye vizuri kwenye michezo.


Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya awali kati ya Simba SC dhidi ya Gendarmerie ya Djibouti, baada ya mchezo alisema kiwango cha mpira nchini kwasasa kimekua hivyo anafuta kauli yake.

''Mchezo umekuwa mzuri na sasa nafuta lile neno (Tanzania ni kichwa cha Mwendawazimu anayejifunza kunyoa atunyoe sisi) lakini sasa sisi ndio vinyozi'', alisema.



Katika mchezo wa jana Simba SC iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 hivyo kujiweka vizuri kwenye mchezo wake wa marudiano huko Djibouti. Yanga pia ilishinda dhidi ya St. Louis ya Shelisheli.

Yanga inayocheza klabu bingwa Africa itasafiri kwenda Shelisheli kwaajili ya mchezo wake wa marudiano Februari 20 huku Simba inayoshiriki Kombe la Shirikisho nayo itasafiri kuelekea Djibouti kwaajili ya mchezo wa Februari 20 au 21.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad