Nandy, Aslay Wapokewa kwa Shangwe na Mwimbaji wa 'Subalkheri' Nyumbani Kwake Zanzibar

Nandy, Aslay Wapokewa kwa Shangwe na Mwimbaji wa 'Subalkheri' Nyumbani Kwake Zanzibar
Waimbaji wawili walioshirikiana kuurudia wimbo ‘Subalkheri’ Nandy na Aslay Ijumaa hii wametua Zanzibar kwaajili ya kukutana na muimbaji wa awali wa wimbo ‘Subalkheri’, Bi. Mwanapombe.

Wawili hao pamoja na team waliyoenda nayo walipokewa kwa shangwe na Bi. Mwanapombe pamoja na familia yake.

Akiongea na waandishi wa habari, Mwanapombe Hiyari alisema amewapokea kwa mikono miwili na baraka tele vijana hao ambao wamewaita kama wajukuu kwa kuwa wameitendea haki kazi yake hiyo.

“Sina shaka na hawa wajukuu zangu, nawaombea dua na wafike mbali zaidi kwenye maisha haya ya Muziki,” alisema Bi. Mwanapombe.

Kwa upande wa Aslay alisema anashukuru Mungu kukutana na mkongwe huyo na kupewa maraka zote katika kazi zao za muziki.

Naye Nandy amesema hata kabla na kuurudia wimbo wa mkoongwe huyo, yeye ni shabiki mkubwa na muimbaji huyo ambaye aliwahi kufanya vizuri na vibao vingi kwa kipindi cha nyuma.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad