Nape Nhauye Awamwagia Lawama Usalama wa Taifa

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye ameibuka na kuituhumu Idara ya Usalama wa Taifa nchini haifanyi kazi zake ipasavyo inavyohitajika na badala yake wamekalia kusikiliza simu za watu wanavyoongea pamoja na kufanya mambo ambayo hayalindi uchumi wa Tanzania.

Nnape ametoa kauli hiyo  jana wakati alipokuwa akichangia bungeni taarifa ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama katika mkutano wa 10 kikao cha nane cha Bunge mjini Dodoma na kuishauri kamati hiyo ipeleke mapendekezo ili waweze kupitia upya sheria ya Usalama wa Taifa na kuiwezesha mikono yao iende mbali, kukumbuka jukumu lao la kuhakikisha wanalinda uchumi wa nchi katika kipindi hichi, ambacho demokrasia ya siasa inahama na kuelekea kwenye demokrasia ya uchumi ambapo muda mwingi wanapaswa kuutumia huko na sio pengine.

Kutoka na hayo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Kapteni George Mkuchika alimjibu Nape na wabunge wengine kwamba kazi ya Idara ya Usalama wa Taifa sio kutafuta watu waliopotea au kuumizwa kama wanavyodai na laiti wangelifahamu wanachokifanya wangekaa kimya.

"Kazi ya usalama wa Taifa nchi yeyote ni kutafuta habari na kuishauri serikali. Kwa kifupi tu mimi nasema hoja mlizozitoa kuhusu idara kwamba haishauri serikali mambo ya uchumi na mambo mengine hamna ushahidi", alisema Kapteni Mkuchika.

Pamoja na hayo, Kapteni Mkuchika aliendelea kwa kusema "sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1996, kazi zilizopitishwa kwa mujibu wa Bunge kuna shughuli nne za idara kwamba ni kukusanya na kutafuta habari pamoja na kuzifanyia tathmini na wanapoyafanya hayo hawayafanyi katika mkutano wa hadhra, kushirikiana na vyombo vya idara nyingine vinashughulikana na usalama wa nchi, kuwashauri Mawaziri ili waishauri serikali na mambo yote ya kuhujumu uchumi na vingine wanayafanya kimya kimya".

Shughuli za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Taifa zimehairishwa jana jioni (Ijumaa) mpaka Aprili 03 mwaka 2018.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad