Nina Uhakika Simba Watasonga mbele, Yanga Wafanye Kazi”-Shaffih Dauda

Vilabu vya Simba na Yanga vinatarajia kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya Afrika leo na kesho michezo ambayo itaamua nafasi ya ya vilabu hivyo kusonga mbele kwenye mashindano.

Simba inashuka uwanjani mucheza mechi ya marudiano dhidi ya Gendarmaie ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa magoli 4-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Dar es Salaam hivyo Simba inahitaji ushindi au sare yoyote ili waweze kusonga mbele.

Yanga wao siku ya Jumatano watacheza mchezo wa marudiano dhidi St Louis ya Ushelisheli wakiwa wanafahamu ushindi au sare yoyote ndio itawafanya kuendelea na mashindano ya vilabu bingwa Afrika.

Mchambuzi wa masuala ya michezo Shaffih Dauda anaamini kwamba Simba wana asilimia nyingi za kuendelea na mashindano kutokana na matokeo waliyopata kwenye mchezo wao wa kwanza lakini anaamini Yanga wanatakiwa kufanya kazi ya ziada ili kusonga mbele.

“Mechi bado hazijamalizika, walicheza dakika 90 bado dakika 90 nyingine. Wote tulishuhudia mechi zilizopita namna ambavyo timu zetu zilicheza”-Shaffih Dauda.

“Yanga walipata matokeo, wamekwenda ugenini. Ushelisheli ni tofauti na ambavyo tuliwazoea zamani, wana timu nzuri na wana mipango, mechi ya nyumbani Yanga walishinda 1-0 kwa hiyo inabidi wafanye kazi kupata matokeo.”

“Simba wana akiba nzuri ya magoli waliyofunga kwenye mechi yao ya nyumbani, nina uhakika Simba watapeperusha vyema bendere ya Tanzania, Djibouti bado wana safari ndefu.”

Kocha wa msaidizi wa Simba Masoud Djuma amesema wachezaji wote wapo sawa kimchezo isipokuwa John Bocco ambaye aliumia kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mwadui pamoja na golikipa Aishi Manula aliyeumia kwenye mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo huo.

“Tutapambana kama kawaida yetu tupate ushindi hapa au matokeo yoyote yatakayotufanya tuendelee mbele”-Masoud Djuma.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad