Okwi Aikutanisha Simba na Waarabu Baada ya Kufanikiwa Hatua ya Kwanza

Okwi Aikutanisha Simba na Waarabu Baada ya Kufanikiwa Hatua ya Kwanza
SIMBA imefanikiwa kutinga hatua ya kwanza ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya jana kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Gendarmarie nchini Djibouti.

Mshambuliaji raia wa Uganda, Emmanuel Okwi, aliifungia Simba bao hilo pekee katika dakika ya 53 na kuifanya Simba sasa kukutana na 'Waarabu' wa Al Masry.

Simba imesonga mbele kwa jumla ya mabao 5-0 kufuatia ushindi wa bao 4-0 walioupata kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.

Al Masry yenyewe pia imesonga mbele kwa jumla ya mabao 5-1 baada ya jana kubanwa na Green Buffaloes na kutoka sare ya bao 1-1 nchini Zambia.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Misri, wenyeji walishinda kwa mabao 4-0.

Simba sasa itakuwa na kibarua mbele ya Waarabu hao, katika kuwania kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo.Timu hizo zitakutana kati ya Machi 6, 7 mwaka huu, huku Simba wakianzia nyumbani kabla ya kuwafuata Al Masry wiki mbili baadaye. 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad