Polisi DR Congo Ahukumiwa Kifungo Cha Maisha Jela Kwa Kuwapiga Risasi Waandamanaji

Mahakama kuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, imemuhukumu kifungo cha maisha askari polisi aliyewafyatulia risasi waandamanaji wanaompinga rais wa nchi hiyo Joseph Kabila.

Polisi huyo ambaye aliwapiga risasi za moto waandamanaji wawili na kuwauwa papo hapo siku ya Jumapili Februari 25, 2018. aliibua hisia kali kwa raia wa Congo baada ya video yake kusambaa mitandaoni.

Waumini wa kanisa Katoliki wakiongozwa na viongozi wao waliandamana katikati ya mji wa Kinshasa wakishinikiza rais Joseph Kabila ang’atuke madarakani.

Kwa mujibu wa mtandao wa Frontline Defenders, Shirika ambalo linafanya kazi chini ya mwavuli wa Haki za Binadamu limeripoti kuwa mpaka sasa zaidi ya watu 35 wanaoandamana kushinikiza Rais Kabila kujiuzulu wameuawa na Jeshi la polisi nchini DR Congo.

Hata hivyo haki za binadamu bado wanadai hukumu hiyo haijatenda haki sawasawa kwani imewaacha wakuu wa Jeshi la polisi.

Chanzo: Frontline Defenders
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad