Polisi sita washikiliwa kwa uchunguzi kifo cha mwanafunzi NIT


olisi inawashikilia askari wake sita na silaha zao kwa ajili ya uchunguzi kuhusu tukio la kuuawa kwa risasi mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akweline.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema hayo leo Februari 18,2018 alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu ulinzi wakati wa kampeni, upigaji kura, na utangazaji matokeo ya uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Kinondoni uliofanyika jana Februari 17,2018.

Amesema polisi iliunda timu ya upelelezi kuchunguza chanzo cha kifo cha mwanafunzi huyo kilichotokea Februari 16,2018 wakati polisi wakiwatawanya wanachama wa Chadema waliokuwa wanakwenda ofisi za mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kushinikiza mawakala wao kupatiwa barua za viapo vyao.


Kamanda Mambosasa amesema polisi pia inawachunguza watuhumiwa 40 ili kubaini iwapo miongoni mwao walikuwepo waliokuwa na silaha za moto.

Amesema pia wanaendelea kuwatafuta wafuasi na viongozi wa Chadema walioshiriki kushawishi wafuasi wao kushiriki kwenye maandamano.  

Wakati huohuo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole katika taarifa aliyoitoa jana Februari 17,2018 alisema chama hicho kinalitaka Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina kuhusu aliyehusika na tukio la kuuawa kwa mwanafunzi huyo.

Polepole alisema polisi imhoji Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na viongozi wenzake walioshiriki maandamano aliyosema hayakuwa halali yaliyosababisha uhai wa Mtanzania kupotea.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad