Polisi nchini Israel imesema Waziri mkuu wa nchi hiyo Benjamin Netanyahu anapaswa kushtakiwa na mashtaka ya rushwa yanayomkabili.
Taarifa iliyotolewa na polisi imesema, wana ushahidi wa kutosha kumtia hatiani Bwana Netanyahu kwa rushwa, ufisadi na kuvunjwa uaminifu katika kesi mbili tofauti.
Waziri mkuu wa Israel anatuhumiwa kwa kutaka gazeti la nchi hiyo la Yediot Aharonot kuchapisha taarifa yake kwa upendeleo, ikiwa kama takrima kulisaidia kuweza kudhibiti magazeti yanayoshindana nayo.
Polisi wanasema mhariri wa gazeti hilo Arnon Mozes naye pia anapaswa kushtakiwa.
Madai mengine ni kwamba Waziri huyo mkuu aliyeongoza nchi hiyon toka mwaka 2009 alipokea zawadi ya kiasi cha dola 283,000 kutoka kwa msanii wa Hollwood Mogul Arnon Milchan na washabiki wengine, ili kuweza kumsaidia kupata Visa ya marekani.
Polisi wanasema Milchan ambaye ni Mtayarishaji wa Filamu naye pia atashtakiwa kwa tuhuza za rushwa.
Akizungumza kupitia Televisheni ya Israel, Benjamin Netanyahu amesema madau hayo hayana msingi wowote na ataendelea kuwa Waziri mkuu wa nchi hiyo.
Hata hivyo upinzani nchini Israel, wamemtaka Netanyahu ajiuzulu kutokana na tuhuma hizo dhidi yake.
Vyombo vya habari nchini Israel vimesema tayari Bweana Netanyahu amehojiwa mara saba.
Uamuzi wa Mwanasheria mkuuu wa serrikali wa juu ya kumshtaki inaweza kuchukua miezi kadhaa.
Uchaguzi wa bunge nchini humo umepangwa kufanyika November mwakani.