Polisi Yakiri Kuwashikilia Waliojeruhiwa Kwenye Maandamano ya Chadema

Polisi Yakiri Kuwashikilia Waliojeruhiwa Kwenye Maandamano ya Chadema
JESHI la Polisi kupitia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Muliro Jumanne limethibitisha kuwashikilia watuhumiwa watatu wenye majeraha ya risasi katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Muliro amesema watuhumiwa hao ni wale waliokamatwa kwenye maandamano ya CHADEMA yaliyofanyika Februari 16 mwaka huu na kusababisha kifo cha mwanafunzi Akwilina Akwilini.

Aidha, kamanda huyo amekanusha taarifa ya kwamba majeruhi hayo hawajapatiwa matibabu tangu wakamatwe, amesema wote wamepelekwa katika hospitali za serikali hivyo hakuna asiyepatiwa matibabu kama inavyoelezwa.

Awali Mbunge wa Mikumi (CHADEMA), Joseph Haule aliandika kupitia Twitter na Facebook kuwa;

“Leo ni siku ya 9, Tangu Kamanda mwenzetu AIDA ULOMI apigwe risasi ya mguu, polisi bado wanamshikilia Kituo cha Oysterbay na wengine kadhaa bado wanashikiliwa kwenye vituo mbalimbali, Hajapelekwa mahakamani, hajapata matibabu yeyote na amegoma kula, twendeni tukamwone na kumsaidia…”
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sasa mtu mmempiga risasi ambapo ni makosa. Bado mnamweka ndani. Ni bahati tu kapona. Angekufa kama Awuilina je. Na sheria zinasemaje. Kwa nini kama mfimfungulie mashtaka. Inabidi yeye awafungulie nyinyi mashtaka kwa kutumia bunduki ovyo.sasa mtawaweka mpaka lini.na kwa kosa gani

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad