Prof. Jay, Nassari Waungana Kuwasaidia Vijana

Prof. Jay, Nassari Waungana Kuwasaidia Vijana
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari na Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule ‘Professor Jay’ wameungana ili kuinua vijana wenye vipaji vya muziki katika jimbo la Arumeru Mashariki.

Mh. Nassari akiongea na Funiko Base ya Radio Five amesema alishaongea na Professor Jay ili aweze kuwasaidi vijana hao wa jimboni kwake kupitia studio yake ya Mwanalizombe.

“Wakati wa kampeni nilimleta Meru na moja ya vitu ambavyo nilimuomba baada ya mimi kushinda wapo vijana kutoka Meru ambao pia wanajihusisha na sanaa na muziki, kwa hiyo nikamuomba ni kwa namna gani anaweza kuwasaidi,” amesema.

“Akaniambia yupo tayari wakafanye katika studio yake lakini kazi wanayotaka kuirekodi iwe na kiwango, sasa mimi siyo mtaalamu sijui kazi gani ina kiwango na ipo haina lakini yeye atawapima na juzi nimeongea naye akaniambia anataka aikarabati ahamishe Mikumi kabisa,” amesema Mh. Nassari.

Kwa upande wake Professor Jay amesema kwa sasa yupo katika mikakati ya kuhamishia studio ya Mwanalizombe Mikumi na imechukua muda kuhuma kutokana wameenda kujenga upya ila kitu ambacho kitakamilika muda sio mrefu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad