Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli leo Ijumaa Februari 23, 2018 amekutana na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na kufanya naye mazungumzo ambapo kwa pamoja wametoa maagizo kwa Mawaziri wao kutatua changamoto ndogo ndogo zinazojitokeza kwenye biashara kati ya Tanzania na Kenya.
Rais Magufuli ambaye wamekutana na Uhuru Kenyatta na kufanya mazungumzo hayo katika Hoteli ya Munyonyo jijini Kampala, amesema wao marais hawana tatizo kwani vitu vidogo vidogo kama biashara ya viatu, nguo, ngano, gesi mawaziri wa nchi mbili wakae wayamalize.
“Kuna mambo madogo madogo yanakuwa yanajitokeza katika biashara kati ya Kenya na Tanzania, tunataka mawaziri wote wa upande wa Kenya na Tanzania mkae muyasolve myamalize, sisi huku juu hatuna tatizo,“amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli yupo nchini Uganda katika Kikao cha 19 cha Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichoanza jana Alhamisi jijini Kampala.
Rais Magufuli, Kenyatta Watoa Maagizo kwa Mawaziri "Mnatakiwa Myatatue Nyinyi, Yasifike Kwetu"
0
February 23, 2018
Tags