RAIS Magufuli: Tunaposikia Kuna Migogoro Kanisani, Huwa Najiuliza sana Tukimbilie Wapi sasa?

Rais Dkt. John Magufuli amesema mara zote anaposikia matatizo yametokea eneo fulani fulani huwa anajiuliza akimbilie wapi ili aweze kupata msaada wa utatuzi wa jambo hilo bila ya kuleta athari yeyote katika taifa.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo (Jumapili Februari 04, 2018) wakati alipohudhuria hafla ya kumweka wakfu na kumsimika Mchungaji Jackson Sosthenes kuwa Askofu wa tano wa Kanisa la Anglikana Dayosis ya Dar es Salaam.

"Sisi viongozi wa serikali mara nyingi huwa tunawategemea viongozi wa makanisa na misikiti katika kutuongoza, nafahamu serikali haina dini lakini naheshimu sana dini na kuthamini mawaidha pamoja na mafundisho yanatolewa na viongozi wa dini wawe waislamu, wakristo hata wahindu tunayaheshimu sana", alisema Rais Magufuli.

Pamoja na hayo, Rais Magufuli aliendelea kwa kusema "siku zote sisi viongozi ndani ya serikali huwa tunafurahi sana kuona makanisa na misikiti ikiwa imetulia, unaposikia mahali fulani fulani kuna migogoro sisi viongozi na hasa mimi huwa najiuliza ninapopata matatizo ntakimbilia wapi. Kwa sababu makanisa na misikiti ni sehemu ya uponyaji wa roho zetu. Uponyaji wa roho ni mahali ambako kuna manufaa zaidi kuliko kwenye uponyaji wa mwili".

Kwa upande mwingine, Dkt. Magufuli amedai endapo mahali kwenye uponyaji wa mwili ukisikia kumeanza matatizo basi unapaswa kutazambua jinsi taifa unaloliongoza roho zake zitakavyopotea.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad