Rais Magufulu Alaani Tukioa la Mwanafunzi Kupigwa Risasa...Atoa Maagizo Haya..


IKULU, DAR: Rais Magufuli amesikitishwa na kifo cha Mwanafunzi wa NIT, Aqulina Akwilini aliyepigwa risasi ktk Maandamano ya CHADEMA

Rais kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter ameviagiza Vyombo vya Dola kuchunguza tukio hilo na kuwachukulia hatua waliohusika kusababisha kifo hicho

Rais pia ametoa pole kwa Familia, Ndugu, Wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT) na wote walioguswa na msiba huu
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ni vizuri unalaani. Lakini umekaa kimya muda wote wa uchaguzi . umeona jinsi tume ilivyowanyima haki wapinzani. Umeshuhudia wagombea wapinzani wakitekwa, kuuawa, na siku mbili tu kabla ya uchaguzi wawili kutokea ufukweni. Moja maiti mmoja kaponea chupuchupu. Ukimya wako kama Raisi na ni kiongozi mkuu wa chama tawala ili kuhakikisha amani, usawa, na usalama na haki inatendeka ungelaumu pale.
    Umeshuhudia jinsi Chadema na Cuf kutokupewa hati zao ile jioni ndicho chanzo cha maandamano. Hukuilaumu tume ya uchaguzi ulikaa kimya. Uliwaambia Watanzania uchaguzi umekwisha sasa kazi tu. Badala yake tumeshuhudia kauli za chama chako tawala kutokana na kukuunga mkono, kwa kutumia slogani ya kukuunga mkono wewe kama raisi , cumekiruhusu chama chako kwa maneno , na matendo na rushwa kuwachukua madiwani , wabunge toka upinzani mkitumia majukwaa ya siasa. Mmeyatumia majukwaa kuwashawisi wabunge na madiwani ambao walishachaguliwa na wananchi nchi kuwatumikia miaka mitano. Kwa kiapo. Mmewapokea haohao kisiasa na mbinu chafu kurudia chaguzi zilezile kwa kutumia pesa za watanzania kunufaisha ccm. Ni matumizi mabaya ya pesa za mtanzania, ni matumizi mabaya ya vyeo mlivyopewa, matumizi mabaya ya sheria. Ni ccm ndiyo inayorudi kwenye majukwaa yale yale kulazimisha watu kurudia chaguzi kwa kujenga maslahi ya chaguzi za 2020. Inamaana bado mko kwenye chaguzi.Badala ya kutupatia katiba eti pesa hakuna hizi pesa za chaguzi na marudio kuikuza na kuitayarisha Ccm kwa uchaguzi ujao mnazitoa wapi. Tumemuona binti mzuri, aliyesoma, na wazazi wamejitahidi kwa hali na mali, yeye ndiye alikuwa mstari wa mbele kwa kujikomboa na kulikomboa taifa , risasi ya polisi imemuua. Hawa polisi nani aliwatuma, kwa nini. Hawa hawa polisi na ccm walishindwa kumlazimisha kiongozi wa tume ya uchaguzi kufuata sheria za nchi hii. Wote watanzania kuanzia raisi, wanasheria, chama tawala kimya.badala ya kuleta usawa, amani, kuhakikisha ulinzi kwa kila mtanzania, uhuru wa uchaguzi bila upendeleo. Mnakaa kimya mpaka moto uwake. Wengi ni wakutuhumiwa. Tume ya uchaguzi, ccm, polisi, wanasheria wote nchini wameshindwa kulinda haki, usawa, kuleta usama mpaka watu wafe. Halafu anayetuhumiwa ni yule anayelilia haki ya mtanzania. Ni lini tutaacha kuigawa nchi na watanzania. Ni lini tutawashika viongozi wetu na kuwalazimisha waone na watende haki. Ni lini viongozi wataamka ili wahakikishe maisha ya mtanzania hata mmoja yatapotezwa kwa ubadhilifu kama huu. Mtu ameshapoteza maisha lini viongozi watamthamini mtanzania na kuthamini maisha ya mtanzania. Kwa nini viongozi wetu wanashindwa au hawataki kuona ukweli wa maisha ya mtanzania. Kwa nini polisi asiwe rafiki wa mtanzania kawaida.kwa nini polisi anapopewa chance ya kuzungumza na mtanzania asiweze kumuona huyu ni ndugu, binadamu kumheshimu, kumjali na kuongea na mtanzania kwa heshima badala ya kuonyesha dharau kwa mtanzania. Mnajenga chuki na mtanzania. Mnaleta uhasama na inamlazimisha mtu kutenda mabaya dhidi ya chama, polisi, na watawala na hata kati ya mtanzania na mtanzania mwenzake. Mnaleta mpasuko nchini hakuna hata kiongozi mmoja anayejaribu kuliunganisha taifa. Watu wanakuogopa raisi wangu wanashindwa kuwa wakwrli. Huru, na wengi wanashindwa kuyatimiza majukumu yao. Badala yake wanajipendekeza na kutaka kukuridhisha wakati wakijua mara nyingi hawakubaliani nawe. Ndo maana hata rushwa haiishi ndani ya chama. Ufisadi hauishi ndani ya ccm sababu mafisadi wakuu bado wapo huko . wakijua hakuna lolote litatokea. Haya yote ni matatizo makuu yanayosababisha uongozozi wako usiwe unavyotarajia. Kuna mapungufu mengi ndani ya mazuri.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad