Ratiba ya Kumwaga Akwilina Yabadirika Hii Hapa Ratiba Kamili

Ratiba ya Kumwaga Akwilina Yabadirika Hii Hapa Ratiba Kamili

Ratiba ya kuaga mwili wa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline imebadilika.

Ratiba ya awali ilieleza kuwa mwili wa mwanafunzi huyo baada ya kutolewa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), ungepelekwa nyumbani kwa dada wa marehemu eneo la Mbezi Louis na mchana kuelekea katika viwanja vya NIT, Mabibo kwa ajili ya kuagwa.

Ratiba mpya iliyotolewa leo Februari 21, 2018 na msemaji wa familia, Festo Kavishe inaeleza kuwa baada ya mwili kutolewa MNH, utapelekwa NIT kwa ajili ya kuagaw.

Kavishe ameiambia MCL Digital kuwa ndugu wataanza safari kuelekea NIT saa 5:00 asubuhi.

Soma: Mwili wa Akwilina kuagwa leo, familia yatoa mchanganuo gharama za Serikali

“Hii ni kwa sababu mazingira ya hapa nyumbani eneo ni finyu. Mpendwa wetu tutamuaga kule NIT saa tano,” amesema.

Amesema nyumbani itafanyika ibada fupi ya wanajumuiya kabla ya kuanza safari kuelekea NIT.

Kifo cha Akwilina kilitokana na kupigwa risasi na polisi Februari 16 akiwa ndani ya daladala eneo la Mkwajuni, Kinondoni jijini Dar es Salaam wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakiandamana kwenda ofisi za mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni kudai viapo vya mawakala wao walioshiriki uchaguzi mdogo wa ubunge Kinondoni, Februari 17.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad