Rapper Rosa Ree amefunguka ishu ya ngoma zake za awali kutopatikana katika official channel YouTube kama ilivyokuwa awali.
Kipindi msanii huyo yupo chini ya label ya The Industry ngoma zake kama One Time, Up In The Air zilipatikana katika channel ya YouTube ya label hiyo lakini tangu aondoke The Industry channel hiyo imefutwa.
Rosa Ree ameimbia Bongo5 ni kitu ambacho anakifahamu toka mwanzo ila hajaamua kukipa nafasi kwa sasa katika muziki wake bali ameamua kujikita katika kutengeneza kazi nyingine mpya na zenye ubora.
“Sijakaa kuwaza hicho kitu kwa sababu kipaji ni kitu ambacho kipo, ni creativity na nina uwezo mkubwa, hizo zilishapita nimefungua channel yangu mpya nina focus for the future.” amesema Rosa Ree.
Pia ameongeza kuwa The Industry wana haki zote kufanya hivyo kwani nyimbo hizo wao ndio wanazimiliki kisheria. Rosa Ree kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Marathon’.
The Industry ni label ambayo ipo chini ya kundi la Navy Kenzo, Label hii ilianza rasmi May, 2016 ikiwa na wasanii watatu, Wildad, Selina na Rosa Ree ila wote hawapo hapo kwa sasa.