Sallam Sk Amuepushia Shari Ruge Baada ya Kusaga Kuingilia kati. Asema 'Tumekataa Kuwa Kaa'

Mtakumbuka siku ya leo, Meneja wa Diamond ametokwa na mapovu balaa akimshambulia mtu ambaye alikuwa hamtaji jina, badae akaahidi kusema ukweli kama alivyoandika hapa => Meneja wa wcb sallam sk atangaza kuachia ukweli wote muda mfupi ujao stay tune

Sasa basi, Sallam SK ameamua kubaki kimya baada ya Joseph Kusaga kumuombea msamaha mtesi wa wasanii ambaye ni Ruge Mutahaba. Pia ametahadharisha kuwa hawawezi kuwa kaa #TumekataaKuwaKaa

Sallam SK ameyaandika haya katika ukurasa wake wa Instagram,

Nanukuu

'Kwa Heshima ya Joe Kusaga kukuombea msamaha kwa leo Bw Ruge Mutahaba naamua kukusitiri, ila ukiendelea kuyafanya ambayo unayafanya basi nitayaanika maovu yako yote unayoyafanya kwenye Industry ya muziki. WCB haina tatizo na media yoyote na wala haina tatizo na Clouds Media Group ila huyu Ruge Mutahaba ndio mwenye tatizo #TumekataaKuwaKa''

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad