Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni (CHADEMA), Salum Mwalimu amemshambulia mgombea mwenzake Maulid Mtulia kwa maneno kuwa kazi ya Mbunge sio kuomba omba wala kulilia bali anapaswa kutetea haki na maslahi ya wananchi katika jimbo lake.
Mgombea huyo ametoa kauli hiyo akiwa kwenye muendelezo wa kuomba ridhaa huku zikiwa zimebakia takribani siku saba ili wananchi wa Jimbo la Kinondoni pamoja na Siha kushiriki zoezi la kupiga kura katika uchaguzi huo mdogo wa marudio na waweze kupata wawakilishi wao ambao kwa mara ya kwanza wataingia bungeni mjini Dodoma Aprili 03 endapo zoezi hilo litakamilika kwa amani na usalama.
"Kazi ya Mbunge ni moja popote pale utakapoenda duniani ambayo ni kusimamia haki, maslahi na mahitaji ya wananchi wake na sio kulilia, kuomba omba, kujiabisha abisha. Ukiwa unauwezo wa kusimamia haki kwa wananchi wako maghorofa yatakuja kwa sababu sio hisani ni haki yao kama walipa kodi", amesema Salum Mwalimu.
Pamoja na hayo, mgombea huyo ameendelea kwa kusema "kama una uwezo wa kusimamia haki na unaujua wajibu wako haiwezekani Mbunge, wananchi wako wanavuliwa nguo kwa kuvunjiwa nyumba, wanakufa, wanadhalilika, heshima ya utu wao inapotea halafu wewe unacheka eti unasema utawajengea maghorofa. Kuna maghorofa makaburini, watu waliokufa utawalipa nini".
Kwa upande mwingine, Salum Mwalimu amedai yeye anajitambua hivyo atahikisha anasimama mbele kupigania haki ya wananchi wa Kinondoni bila ya kujali ni wakati gani uliokuwepo muda huo.
When you vote me i'll do this i will do that the same"fucking old story" it makes me go mad madly
ReplyDelete