Sare na Mwadui Yamtoa Povu Haji Manara

Sare na Mwadui Yamtoa Povu Haji Manara
Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano ndani ya klabu ya Simba Haji Manara amesema Simba sio timu ya kwanza kutoa sare au kufungwa na Mwadui hivyo mashabiki wasiongee sana.


Kupitia moja ya kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii Manara ameandika ujumbe ambao unaonekana kuwa povu kwa mashabiki wa wapinzani wao huku akiweka wazi kuwa sare ya jana dhidi ya Mwadui FC kamwe haijaitoa Simba kwenye njia.

''Simba haitatoka mstarini na washabiki wetu tulieni na wajibu wenu ni kuiombea timu na kuisuport'', ameandika Manara ikiwa ni chini ya siku moja tangu timu hiyo itoe sare ya 2-2 dhidi ya Mwadui ugenini Shinyanga.



Aidha Manara ameongeza ''Mwadui imezifunga Singida United na kabla yetu sisi waliwafunga Mtibwa 3-1 kule Shinyanga, wametoka sare na Yanga na Azam tena wakiwa kwao Dar, hizo ndio 'big five' kwenye ligi kwa sasa, sisi kutoka nao sare kwao 'why' iwe nongwa tena ugenini'', ?.

Baada ya sare ya jana Simba imefikisha alama 42 ikiwa kileleni kwa alama 5 zaidi ya Yanga ambayo inashika nafasi ya pili ikiwa na alama 37 huku Azam FC ikishika nafasi ya tatu ikiwa na alama 34.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad