SERIKALI imesisitiza kwamba itaendelea kuimarisha mifumo yake ya utoaji huduma za dawa kutokana na ukweli kwamba ya dawa zinatumika kwa wanyama na binadamu na kuleta usugu wa ugonjwa
husika kwa mgonjwa na gharama kubwa kwa taifa.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Dr Faustine Ndugulile wakati wa Ufunguzi wa mkutano wa Kimataifa wa siku nne wa Jukwaa la kudhibiti usambazaji na uzalishaji wa bidhaa za madawa Afrika ambapo nchi 18 zipo nchini kujadili namna bora ya kudhibiti madawa yasiyo na viwango katika soko ili kuimarisha na ustawisha afya za wananchi wake.
“Tanzania ni moja ya nchini iliyofanikiwa kwa kiasi kikubwa katika udhibiti wa dawa feki kwa Afrika nzima na mamlaka ya dawa na vipodozi nchini ina maabara za kisasa na watalaamu wa kutosha wa kuweza kufanya ukaguzi wenye ubora na viwango vya kimataifa,” amesema Ndungulile.
Ameongeza kwamba Tanzania imeweza kujitosheleza kwa dawa za kutosha na zenye viwango vya kimataifa na changamoto kubwa ilikuwa kudhibiti dawa zinazoingia kwa njia ya panya ambapo tayari mamlaka husika wameshafungua ofisi za kanda ambazo zimefanya kazi kubwa kupunguza mianya ya dawa zinazoingia kwa njia ya panya.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Bi Agnes Kijo amefafanua kwamba wataalamu kutoka nchi za Cameron, Ivori Coasti, Mali, Nigeria, Ghana, Burkina Faso, Mauritius, Senegal, Ethiopia, Sudan, Guinea, Sierra Leone, Uganda, Malawi, Zambia, Zimbabwe na Afrika kusini watakutana kwa siku nne ili kuja na mpango kabambe wa kudhibiti dawa bandia.
“katika mkutano huu jambo kuu litakuwa na kwa namna ngani tunaweza kudhibiti dawa bandia kwenye masoko na kuhakikisha kwamba wazalishaji pia wanatoa dawa zenye ubora unaokubalika katika soko,”
amesema Kijo.
Kijo ameongeza kwamba TFDA kwa sasa ina maabara 24 nchi nzima zenye vifaa vya kisasa vya kufanya ukaguzi
nchini nzima na ofisi saba za kikanda ambazo zina wataalamu wa kutosha kuweza kuhudumia sehemu za mikoani.