Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas, amesema hali ya uchumi wa Tanzania imeimarika ikilinganishwa na awamu zilizopita ambapo imeshika nafasi ya 48 kwa nchi zenye uchumi jumuishi duniani, pia ni ya pili Afrika ikifuatiwa na Tunisia ambapo kusini mwa jangwa la Sahara ni ya kwanza.
Abbas alikuwa akizungumza leo jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari ambapo mambo mengine aliyozungumzia ni kuhusu kifo cha mkongwe wa siasa nchini marehemu Kingunge Ngombale-Mwiru aliyemuita kuwa ni msahafu wa siasa za Tanzania.
Pia Abbas alitumia fursa hiyo akisema kwamba atakuwa na utaratibu maalum wa kuzungumza na waandishi wa habari kila mwisho wa mwezi ambao utatolewa karibuni.