Serikali ya Botswana ilisema Jumatatu ilimlaumu Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kwa kuwa kiini cha ukiukwaji wa haki za binadamu na kuzorota kwa hali ya usalama.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imemkosoa Kabila kwa kuendelea kungÆangÆania madarakani huku ikitoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuongeza shinikizo dhidi ya kiongozi huyo ambaye alipaswa kuondoka madarakani Desemba 2016.
Mbali ya Botswana kumlaumu Kabila, pia imewakosoa viongozi wengine wa Afrika ambao wameamua kubadili Katiba za nchi zao ili waendelee kubaki madarakani.
Viongozi hawa sasa wameamua kutumia njia kama vile kuchelewesha kufanya chaguzi au mabadiliko ya Katiba za Taifa kwa lengo la kuendelea kubaki madarakani,ö ilisema taarifa hiyo.
ôNi wazi kwamba viongozi kama hawa wanaongozwa na maslahi yao binafsi badala ya kujali maslahi ya taifa. Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ni mfano kuntu. Tunaendelea kushuhudia kuzorota kwa haki za binadamu katika nchi hiyo na sababu kubwa ni kiongozi wake mkuu kuendelea kuchelewesha uchaguzi huku akiwa amepoteza udhibiti wa vyombo vya usalama.ö
Botswana ina uthabiti wa kimaadili wa kuzinyoshea kidole nchi nyingine kwa sababu Rais wake Ian Khama aliyeingia madarakani mwaka 2008 alitangaza Novemba mwaka jana kuwa atangÆatuka Aprili mwaka huu na kumwachia ofisi makamu wake Mokgweetsi Masisi kuongoza hadi uchaguzi mkuu mwaka 2019
Khama alichukua nafasi ya Festus Mogae kama rais mwaka 2008 baada ya kutumikia kama makamu wa rais kuanzia 1998. Mwaka 2009 alichaguliwa kuwa rais na aliongoza kipindi cha kwanza cha miaka mitano na mwaka 2014 alishinda kipindi cha pili na cha mwisho.
Lakini baadhi ya nchi kama vile Rwanda na Uganda zimebadili katiba zao kuwaruhusu viongozi wa sasa kutawala zaidi ya mihula miwili ya kikatiba na Burundi inahaha kubadili katiba.
Kabila aliingia madarakani mwaka 2001 akichukua nafasi ya baba yake Laurent DΘsirΘ Kabila aliyeuawa na walinzi wake.
Kutokana na Kabila kutotaka kuondoka yamekuwa yakifanyika maandamano nchi nzima kumtaka ajiuzulu lakini amekuwa akituma vikosi vya usalama kuzima hali iliyosababisha vifo na majeruhi.
Botswana ni nchi pekee Africa isiyokuwa na siasa za Kinafiki.They call a spade by its name!.
ReplyDeleteSisi tumeiingiza South Sudan katika EAC na tumeshindwa kumwambia raisi Kiir kuwa ni sehemu ya matatizo na anapaswa kukaa pembeni for sake of peace.