Serikali ya China Yaridhia Kutoa Bilioni 138 Kwaajili ya Ujenzi wa Chuo Kikuu

Serikali ya China Yaridhia Kutoa Bilioni 138 Kwaajili ya Ujenzi wa Chuo Kikuu
February 12, 2018 Good News niliyoipokea toka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais ni kuhusu serikali ya China imeridhia kutoa msaada wa Dola za Marekani Milioni 62 sawa na Shilingi Bilioni 138.3 za Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Usafirishaji hapa nchini.

Balozi wa China hapa nchini Wang Ke amesema hayo leo February 12, 2018 muda mfupi baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na kumkabidhi barua yenye ujumbe wa Rais wa China Xi Jinping, Ikulu Dar es Salaam.

Wang Ke ameeleza kuwa msaada huo ni sehemu ya misaada na miradi mbalimbali ambayo China inaitekeleza hapa nchini Tanzania yenye lengo la kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati yake na Tanzania.

President Magufuli amemuomba Wang Ke kumfikishia shukrani zake kwa Rais wa China kwa ujumbe na msaada huo ambao amesema utasaidia kuimarisha huduma za usafirishaji hapa nchini.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad