Serikali ya Kenya Yashtakiwa kwa Kufungia Vituo vya TV kwenye ‘kuapishwa’ Raila

Serikali ya Kenya Yashtakiwa kwa Kufungia Vituo vya TV kwenye ‘kuapishwa’ Raila
Mwanaharakati nchini Kenya Okiya Omtatah amefungua mashtaka dhidi ya serikali katika Mahakama Kuu kutokana na uamuzi wake wa kuzima vituo vya televisheni vya Citizen TV, NTV na KTN pamoja na Inooro TV siku ya ‘kujiapisha’ Kiongozi wa Upinzania NASA Raila Odinga.

Omtatah ameeleza kuwa kufungiwa kwa vyombo hivyo vya habari  ni kinyume cha sheria na hakuna sheria yoyote iliyowapa mamlaka ya kutekeleza suala hilo.

Amedai kuwa serikali hiyo lazima izuiwe katika kudharau utawala wa sheria jambo ambalo ni msingi mkuu wa thamani ya taifa na kanuni ya utawala.

Ameongeza kuwa anahitaji mahakama iamuru serikali ilipe fidia vyombo hivyo vya habari vilivyofungwa na kusababishiwa hasara kutokana na jambo hilo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad