Sheik Mkuu Amtolea Uvivu Mange Kimambi "Huu Ndio Mwaka Wake wa Mwisho"

Sheik Mkuu Amtolea Uvivu Mange Kimambi "Huu Ndio Mwaka Wake wa Mwisho"
Sheik Mkuu Mkoa wa Dar es Salaam Al Haji Mussa Salimu amtolea uvivu mwanadada maarufu mitandaoni mange Kimambi amwambia huu ndio mwaka wake wa mwisho  kutumia mdomo wake kuwatukana watu haswa viongozi.

"Kuna watu wanatafuta umaarufu  kupitia midomo michafu , mimi siwezi kupigia kampeniCCM sasa tunamwambia huyu anayeitwa @mangekimambi acjeze na watu wengine na si viongozi wa dini huu ndio mwisho wake tutasema na mwenyezi mungu na Majibu Mtayaona

Sheikh huyo amesema kwamba kutokana na kitendo hicho cha Mwanadada huyo kumuanika mtandaoni na kumtolea maneno machafu yeye kama kiongozi wa dini atarudi kwenda kushtaki katika mahakama ya mbinguni ambayo haina rushwa.

Kauli hiyo ya Sheikh Mkuu imekuja ikiwa ni siku moja tangu ianze kusambaa picha yake mitandaoni na kuanza kutuhumiwa kuwa anashiriki katika kampeni za uchaguzi mdogo kukisaidia Chama Cha Mapinduzi

"Tutarejea katika mahakama ya mbinguni kwani mahakama ya Mwenyezi Mungu haina rushwa na tutamuuliza  Mwenyezi Mungu kama alimpa Huyu Mange Kimambi ulimpa mikono kwa ajilli ya kudhalilisha na kuvunja heshma za watu. Amekuwa akiwatukana viongozi wa serikali lakini kwa hekima zao wamemnyamazia kimya" Al Haji Mussa Salimu .

Ameongeza kwamba "Tunamuonya acheze na namba nyingine lakini siyo viongozi wa dini kwani wao wana mahakama ya kushatakia. Huu utakuwa mwaka wake wa mwisho kutumia ulimi au mikono yake kudhalilisha watu".

Hata hivyo Sheikh huyo amesema kwamba wapo watu wengi waliompa rai ya kutomjibu Mange Kimambi  na kwamba kumjibu kwake kutamfanya atukanwe sana laki amesema kwamba mwanadada huyo aendelee kutukana kwani dua ya mwenye kudhulumiwa haina kizuizi na kama anaishi hapa duniani basi afahamu kwamba hataendelea kuwa salama na amejihalalishia mwenyewe kwa ulimi wake na mikono yake.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. MTOTO-AKILILIA-WEMBE-MPE.........!!

    ReplyDelete
  2. Sheikh Mkuu yupo sahihi kabisa Mahakama ya mbinguni haina RUSHWA lakini mimi nnaimani kabisa bila shaka yeyote tayari Mahakama ya mbinguni imeshaanza kumuhukumu Mambe kimange kwani vitendo anavyoendelea kuvifanya vya kutukana watu na hasa viongozi wa dini ni vitendo vinavyofanywa na mtu alielaanika. Aidha yeye mwenyewe kimange au washishirka wake waliojificha nyuma ya jina lake tayari Mahakama ya mbinguni imeshaanza kuwahukumumu na sasa wanawatukana viongozi wa dini na waumini wao ni hatari kabisa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad