Siku ya 100: Azory Gwanda Yuko Wapi?

Siku ya 100: Azory Gwanda Yuko Wapi?
Ni siku 100 tangu kutoweka kwa Mwandishi Azory Gwanda wa gazeti la Mwananchi nchini Tanzania aliyetoweka mwezi wa November mwaka jana.

Francis Nanai Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications, MCL, amesema wataisaida familia ya mwandishi huyo kwa kulipia ada za watoto,bima ya afya na mtaji biashara kwa mke wa Azory ili aweze kujikwamua kiuchumi.

Mpaka sasa MCL hawana ripoti yoyote toka chombo chochote cha ulinzi na usalama juu ya kupotea kwa Azory.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa awali na kampuni ya magazeti ya mwananchi, mwanahabari huyo wa kujitegemea alitoweka tarehe 21 Novemba.

Bw Gwanda alikuwa anaishi na kuripoti kutoka mji mdogo uitwao Kibiti, ambao upo kilomita kama 130 hivi kusini mwa Dar es Salaam.

Bwana Gwanda ni mmoja wa waaandishi wa kwanza kabisa kuripoti kwa kina juu ya mfululizo wa mauwaji yaliyokuwa yakitekelezwa na watu wasiojulikana yaliyowalenga polisi na viongozi wa mji huo.

Mauwaji hayo yaliyotokea miezi kadhaa tu iliyopita yalitia hofu kubwa mjini hapo.


Mke wake Anna Pinoni alisema watu wapatao wanne wakiwa kwenye gari aina ya Toyota Land Cruiser nyeupe walimchukua bwana Gwanda kutoka katikati ya mji huo, mahali ambapo hupendelea kukaa.

Anasema pia aliporudi nyumbani alikuta vitu vimezagaa, ishara kwamba inawezekana waliipekua nyumba yao.

Bw Azory aliwasiliana na ofisi za Mwananchi mara ya mwisho tarehe 20 Novemba kwa majukumu ya kikazi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad