Simba Wamuacha Asante Kwasi

Simba Wamuacha  Asante Kwasi
KIKOSI cha Simba kimewasili salama jijini Mwanza asubuhi kwa ndege tayari kwa ajili ya kuwakabili wapinzani wao Mwadui FC huku wakimuacha beki wao kiraka Mghana, Asante Kwasi.

Simba inatarajiwa kuvaana na Mwadui kesho Alhamisi kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga katika mechi ya Ligi Kuu Bara mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkubwa.



Katika mechi hiyo, Simba wataingia uwanjani wakiwa na morali ya hali juu baada ya kuanza vizuri michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuwafunga Gendarmerie ya Djibouti mabao 4-0.



Akizungumza na Championi Jumatano, Kocha Msaidizi wa Simba, Mrundi, Masoud Djuma alisema wanashukuru kikosi chao kimefi ka salama kikiwa na morali ya hali ya juu katika kuhakikisha wanarejea jijini Dar es Salaam na pointi tatu.



Djuma alisema, msafara huo umeondoka na wachezaji wote isipokuwa Kwasi anayetumikia adhabu ya kadi tatu za njano alizozipata kwenye mechi zilizopita za ligi kuu.



“Tumewasili salama mkoani Mwanza kwa ndege na kuelekea Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa keshokutwa (kesho) dhidi ya Mwadui na jambo la kushukuru kwetu kama benchi la ufundi kuwa wachezaji wetu wako fi ti kwa ajili ya mechi hiyo.



“Kwasi tumemuacha Dar es Salaam kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano alizozipata kwenye michezo iliyopita ya ligi kuu.



“Hivyo, kama benchi la ufundi tukiongozwa na bosi wetu Lechantre (Pierre) tayari tumeanza kumuandaa Tshabalala (Mohamed              Hussein) kwa kumpa mbinu za uchezaji kama unavyojua Kwasi alikuwa ashauzoea mfumo mpya wa kocha unaohitaji kukaba na kushambulia ndani ya wakati mmoja,” alisema Djuma.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad