“Ni bahatika kuiyona mechi ya leo, ilikuwa nzuri sana unaiyona Simba SC kama timu ambayo kweli ilikuwa kambini na ina mwalimu na uwelewano wa hali ya juu.”
“Mechi ulikuwa nzuri sana nimefurahia na kama kiwango cha mchezo wa mpira Tanzania kitakuwa hiki kama alivyosema mzee wetu Ali Hassan Mwinyi sisi siyo tena kichwa cha mwendawazimu ila cha muungwana ambacho kila mtu lazima akisogelee kwa uwangalifu mkubwa sana.”
Waziri Mwakyembe alipo ulizwa kuhusu malalamiko ya Yanga SC kukosa nafasi ya kufanya mazoezi siku moja kabla ya mechi yao ya kimataifa dhidi ya St Louis amesema
“Niwashauri Yanga SC kwamba akili yao yote ikazanie mechi ya marudiano inayo kuja waache mambo ya kulalamika hakuna dawa hakuna muarubaini ya kushinda ni mazoezi na timu kuweza kuelewana nimeona gonga safi za leo za Simba SC kwa kweli nimeona goli zaidi ya saba ila kwa bahati mbaya sana yamekwenda manne.”
“Kuhusu Yanga SC kulalamika sisi hatujapata malalamiko rasmi ila nimeyaskia bungeni watu wakisema lakini cha msingi ni kwamba wote mnajua uwanja wetu wa taifa umetoka kwenye ukarabati mkubwa sana tumekabidhiwa ukiwa na garantii wa kuweza kuutumia kwa zaidi ya miaka 10 bila kuweka nyasi mpya lakini una masharti yake.”
“Huwezi ukawa na mechi kubwa tatu kwa wiki katika uwanja huu ukifanya hivyo hatuwezi kuwa nao kwa zaidi ya miaka mitatu ijayo.”
“Kilichotokea wiki hii tulikuwa na mchezo wa Azam FC na Simba SC wiki hii moja, huku tukijua tuna mechi mbili za kimataifa na katika mchezo huo timu ngeni inapewa kipau mbele katika uwanja ule ule ambao niwa wenyeji kwa upande wa timu hizi Yanga SC na Simba tulichukulia wana ujua.”
Waziri Mwakyembe amezitaka klabu hizi kongwe Yanga SC na Simba SC ambazo zina umri wa zaidi ya miaka 80 kuwa na viwanja vyao.
Tungemuomba Waziri Mwakyembe kwa kuwa hii awamu ya tano ni awamu ya maendeleo na uwazi na kwa hakika watanzania wengi wanaamini serikali hii ikilisimamia jambo linakuwa basi ingekuwa busara sana kuvipatia hivi vilabu viwili vikongwe ushauri nasaha au hata msaada kuhakikisha vinakuwa na miundo mbinu yake hasa ya viwanja. Hivi vilabu viwili simba na yanga hakuna ubishi sio masuala ya mchezo tu bali vimo miongoni mwa tamaduni za mtanzania. Serikali ilitakiwa kuwekeza zamani tu katika vilabu hivi kwani hakuna hasara pale hivi vilabu vina idadi kubwa ya watu wanaovishabikia na nnaamini chini ya usimazi makini na tunaamini serikali ya Magufuli ni serikali makini. Kama kungekuwa na vivutuo vya ndani vya kitalii ambavyo vingepata kutembelewa na watu wengi wa ndani hata wa nchi jirani basi viwanja vya uhakika vya vilabu hivi viwili vingekuwa miongoni mwa vivutio vikubwa kabisa nchini.
ReplyDelete