Siri Yavuja..... Kumbe Dokii Alikua Aolewe na Marehemu Mowzey Radio

Siri Yavuja..... Kumbe Dokii Alikua Aolewe na Marehemu Mowzey Radio
UKIPEWA ubuyu wa Zenji sharti uumun’gunye wenyewe mdomoni bila kitu kingine. Kufuatia kifo cha mwanamuziki wa Uganda, Mowzey Radio kilichojiri mwishoni mwa wiki iliyopita, ubuyu wa motomoto mjini unabumburua kwamba, kumbe mkongwe wa maigizo Bongo, Ummy Wenslaus ‘Dokii’ alikuwa aolewe na jamaa huyo.

Ubuyu huo uliochambuliwa vyema na Ijumaa Wikienda ulidadavua kwamba, Dokii alikuwa na uhusiano wa siri wa kimapenzi na Radio ambaye pia alikuwa ni prodyuza maarufu wa muziki nchini Uganda.
RAFIKI WA KARIBU ATHIBITISHA

Rafiki wa karibu wa Dokii alilithibitishia gazeti hili kuwa, Dokii na Radio walikuwa na uhusiano wa kimapenzi na kwamba walikuwa wakipendana mno.

Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kwamba, kuna kipindi Radio alitimba Bongo kwa ajili ya ziara ya kimuziki ambapo alifikia nyumbani kwa Dokii, Kigamboni jijini Dar.

“Ninajua kabisa Dokii atakuwa ameumizwa sana na kifo cha Radio ingawa hawezi kuweka wazi kwa kila mtu, lakini kiukweli ameumia sana,” alisema rafiki huyo wa Dokii.




Msambaza ubuyu huyo aliendelea kutiririka kuwa, kuna kipindi Dokii alishika ujauzito wa Radio na marafiki zake wote wakajua.

“Wakati Dokii akiwa mjamzito kulitokea kutokuelewana kati yao na hapo ndipo mimba ikayeyuka, lakini kama si hivyo sasa hivi Dokii angekuwa na mtoto wa Radio,” alizidi kumwaga ubuyu rafiki huyo na kuongeza:

“Walikuwa kwenye hatua za mwanzo za kuoana maana Dokii alikuwa hakauki Kampala (Uganda).”

TUMFUATE DOKII KIGAMBONI

Baada ya kupata ubuyu huo, Ijumaa Wikienda lilisaga soli hadi Kigamboni kumsaka Dokii ili aeleze ukweli juu ya jambo hilo ambapo alipopatikana, mambo yalikuwa hivi;

Ijumaa Wikienda: Dokii mambo vipi? Nilidhani upo Uganda!

Dokii: Uganda? Kuna nini huko?

Ijumaa Wikienda: Si kwenye mazishi wa Mowzey Radio?
Dokii: Jamani we’ acha tu, aisee ameniuma sana yule kaka, sijaenda, lakini unajua yule jamaa tumesoma shule moja ya muziki Uganda, tunafahamiana vizuri sana.

Ijumaa Wikienda: Nilijua usingekosa kwenda kwani kuna taarifa kuwa pia alikuwa mchumba wako!

Dokii: (anaguna) nani amekuambia? Kweli ninyi ni mapaparazi. Ndiyo ilikuwa hivyo, lakini hapa juzikati tulikuwa mbali kidogo maana tuligombana.

Ijumaa Wikienda: Kuna madai kuwa uliwahi kushika mimba yake, je, hilo likoje?



Dokii: Uwii…vitu hivyo nani amekuambia? Ilikuwa hivyo, lakini tumuache apumzike sasa.

Radio alikutwa na umauti mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kupoteza fahamu kwa siku kadhaa kufuatia kupigwa na baunsa alipokuwa klabu jijini Kampala, Uganda. Alitarajiwa kuzikwa wikiendi iliyopita jijini humo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad