Nahodha wa Simba John Raphael Bocco ‘Adebayor’ jana Januari 4, 2018 alifunga magoli mawili dhidi ya Ruvu Shooting na kufikisha jumla ya mabao tisa kwenye ligi msimu huu akiwa nyuma kwa magoli matatu dhidi mshambuliaji mwezake Emanuel okwi anaeongoza orodha ya wafungaji akiwa na magoli 12 hadi sasa.
Shaffih Dauda amesema kutokana na anavyomfahamu Bocco hashangazwi kuona mchezaji huyo wa zamani wa azam akipata matokeo mazuri akiwa fit kwa sababu ni miongoni mwa wachezaji wachache wazawa wanaothamini kazi yao.
“Bocco ni moja ya wachezaji wenye nidhamu ya hali ya juu, ni mchezaji ambaye kwa kumfuatilia kwangu na ninavyomfahamu, anaithamini kazi yake. Ni mchezaji anayejua anatakiwa kufanya nini uwanjani na nje ya uwanja.”
“Wakati yupo azam, inatokea wachezaji wamemaliza mazoezi na kupewa mapumziko ya siku mbili nyumbani kabla ya kurejea tena azam complex kuweka kambi kujiandaa na mechi, bocco alikuwa anabaki azam complex anaendelea kujifua mwenyewe, anaungana na vijana wa u20 kufanya mazoezi wachezaji wenzake wakirui baada ya siku mbili wanamkuta anaungana nao.”
“Ubora wa bocco sio kitu kinachokuja kwa bahati mbaya, anawekeza muda na ananidhamu ya juu, ni nahodha ambaye anakuwa wa kwanza katika tukio lolote linalohusu timu. Basi la timu likiwa linaondoka kwenda mazoezini bocco atakuwa ameshakaa kwenye siti zamani, mazoezini na kwenye chakula cha pamoja mara nyingi anakuwa wa kwanza, kwa hiyo sishangai kuona anapata matokeo mazuri anapokuwa fiti.”
Bocco amekuwa na mwendelezo mzuri wa kufunga mfululizo katika mechi za hivi karibuni, alifunga magoli mawili vs Ndanda, alifunga goli moja vs Kagera Sugar, alifunga magoli mawili vs Majimaji, alifunga magoli mawili vs Ruvu Shooting.