Sugu Bado Asugua Jela.. Atembelewa na Wabunge wa Chadema, CUF Mahabusu

Wabunge wamefika Gereza Kuu la Ruanda jijini Mbeya kumjulia hali mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi 'Sugu'.

Waliomtembelea Sugu ni mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema na wa Tandahimba (CUF), Katani Katani.

Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wapo mahabusu wakikabiliwa na kesi ya kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.

Lema na Katani wakiongozwa na mwenyeji wao Mbunge wa  Viti Maalumu, Sophia Mwakagenda pia wamefika nyumbani kwa Desderia Mbilinyi, mama mzazi wa Sugu eneo la Sae jijini Mbeya kwa ajili ya kumfariji na kumtia moyo kutokana na misukosuko anayopitia mtoto wake.

Wakizungumza na familia ya Sugu, wabunge hao wamesema yupo gerezani kwa kuwa anapigania haki za wananchi.

Lema amemtaka mama huyo kuwa na moyo wa uvumilivu.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Anakiburi na dharau kwa serikali, hata Faru porini na nguvu zake huwa na common sense ya kumuheshimu Simba licha ukweli ni Kwamba Faru akipotea step anaweza kuliwa lakini Simba ndie mwenye serikali ya wanyama na bila ya Simba porini kuna uwezekano mkubwa ya binaadamu wangelifanya wanavyotaka kwa wanyama wengine na hapana shaka yeyote sisi binaadamu ndio adui mkubwa hata kwa Dunia tunayoishi. la msingi ni kuelezana ukweli yakwamba sehemu yeyote lazima kuwe na mamlaka na mamlaka yasiogopewe lakini lazima yaishimiwe ili kuleta utulivu kwenye jamii yeyote ile .

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad