TAKUKURU imeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa hawaicheleweshi kwa makusudi kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili aliyekuwa Rais wa (TFF), Jamal Malinzi na wenzake bali jalada lipo kwa DDP.
Mbali na Malinzi, washtakiwa wengine ni Katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa shirikisho hilo, Msiande Mwanga.
Wakili wa TAKUKURU, Leornad Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na jalada lipo kwa DDP analipitia ili atoe kibali cha usikilizwaji wa kesi hiyo.
Hata hivyo, Wakili wa utetezi Abraham Senguji amedai ni miezi 8 hadi sasa wateja wao wapo gerezani, hivyo anaomba upande wa mashtaka uharakishe upelelezi.
Baada ya kueleza hayo, Swai alidai kuwa hawacheleweshi upelelezi wa kesi hiyo kwa kusudi bali jalada lipo kwa DDP analipitia hivyo anaomba kesi iahirishwe hadi tarehe nyingine.
Baada kueleza hayo, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi March 1,2018 kwa ajili ya kutajwa.
Washtakiwa kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 28, ikiwemo ya utakatishaji fedha ambazo ni Dola za Marekani, 375,418.
Takukuru: Hatucheleweshi Kesi Inayomkabili Malinzi Bali Jalada Lipo kwa DPP
0
February 22, 2018
Tags