Tanzia: Hakimu Afariki Dunia Ghafla

Tanzia: Hakimu Afariki Dunia Ghafla
Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Juma Hassan Kasailo amefariki dunia ghafla jana jioni Februari 23, 2018.

Taarifa za kifo cha hakimu huyo zimethibitishwa na Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Ilvin Mugeta.

"Mimi niko safarini, lakini ninazo taarifa hizo kuwa Hakimu Kasailo amefariki dunia,” amesema Mugeta leo Jumamosi Februari 24 alipozungumza na MCL Digital.

Kasailo atazikwa kesho Jumapili Februari 25, saa 7:30 mchana Segera kwa Msisi, wilayani Korogwe mkoani Tanga. Mwili wa marehemu unaagwa leo mchana nyumbani kwake, Chanika Buyuni jijini Dar es Salaam.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad