Tausi Awapa Makavu Wanaomsema Vibaya Kuhusu Mavazi Yake

Tausi Awapa Makavu Wanaomsema Vibaya Kuhusu Mavazi Yake
Msanii wa filamu nchini Tanzania na Rais wa watoto, Tausi Mdegela amefunguka na 'kuwachamba' watu wanaomsema vibaya kuhusiana na mavazi yake anayovaa na kudai kama inawakera basi wakanunue nguo wampelekee na sio kumpangia cha kuvaa.


Tausi ametoa kauli hiyo kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kwenye ukurasa wa facebook wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana mpaka saa 10 alasiri baada ya baadhi mashabiki zake wakimshambulia kuhusu nguo zake katika mitandao ya kijamii.

"Mimi ni Tausi na nitabaki kuwa Tausi tuu, nivae joho, pensi hata taiti ni mimi tu. Kwa hiyo mtu hawezi kunipangia maamuzi kuhusu mavazi eti usivae hichi vaa kile. Niletee dera halafu chukua zile pensi choma 'simple' tu", amesema Tausi.

Pamoja na hayo, Tausi ameendelea kwa kusema "kwa sababu mimi nimenunua hiyo pensi yangu ni hela ambayo niliyokuwa nayo hiyo siku nikaona nisiondoke mikono mitupu nikanunua hiyo pensi. Wewe ambaye inakukwaza niletee nguo ambayo unahisi nitapendeza tofauti na ninavyovaa".

Kwa upande mwingine, Tausi amedai kama mpenzi wake akimsifia kuwa amependeza kutokana na mavazi aliyoyavaa hawezi kumpa nafasi mtu mwingine kumsikiliza juu ya alichokivaa.

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tausi umetisha mama.
    Isingekuwa Hemedi Phd. Mie ningekuoa Tausi wangu.
    Nakupenda jinsi unavyo pendeza.. Ila sina Jinsi... Ajili wewe ni wa watu.
    Niambie kama nafasi bado ipo.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad