Timu ya Azam Yaweka Kambi Chamanzi

Timu ya Azam Yaweka Kambi  Chamanzi
Klabu ya soka ya Azam FC imesema haina mpango wa kuweka kambi nje ya uwanja wake wa Azam Complex kwaajili ya kujiandaa na mchezo wake dhidi ya Simba SC.


Msemaji wa klabu hiyo Jaffary Idd amesema kuwa timu imeanza kambi jana Jumapili kwenye makao makuu ya klabu hiyo Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam ikiwa ni maandalizi ya mwendelezo wa mechi za ligi ikiwemo ya Simba jumatano.

''Sisi kama Azam hatuna pakwenda, wala hatutaenda Bagamoyo au Zanzibar zaidi tutakuwepo hapahapa Azam Complex  tutajiandaa na kuondokea hapa kuelekea uwanja wa taifa kwaajili ya mechi'', amesema.

Simba na Azam zinakutana katika mchezo wa raundi ya 17 ya ligi kuu soka Tanzania Bara ambapo mchezo wa kwanza utapigwa kwenye dimba la taifa jiji Dar es salaam. Katika mchezo wa raundi ya kwanza kwenye uwanja wa Azam Complex timu hizo zilitoka sare.

Kwa upande mwingine Jaffary Idd amesema kwasasa timu yao ina kikosi kipana licha ya kuwa na majeruhi kadhaa lakini wanaamini waliopo watafanya vizuri. Pia amesema walimu wamelifanyia kazi suala la ufungaji na ndio mana katika mechi zao mbili za mwisho wamefunga mabao nane.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad