Uchaguzi Kinondoni: Mwanafunzi wa Mwaka wa Kwanza UDSM Apoteza Maisha!

Wakati CHADEMA wanaelekea kweny ofisi ya mkurugenz kudai barua za viapo..polisi walivuruga na kuanza kupiga mabomu zikiambatana na risasi za moto..kwa wapenzi na wanachama wa CDM eneo la mkwajuni..kuna polisi alifyatua risas ambayo ilimlenga mwanafunzi wa mwaka wa kwanza UDSM Aqulina Akwilini..risas iliyomlenga kifuani na kupoteza maisha

Mtatiro ameandika;

DAMU!

Kwa mujibu wa sheria za uchaguzi, msimamizi wa uchaguzi wa jimbo analo jukumu la kutoa viapo kwa kila wakala wa kila chama cha siasa ambaye atakwenda kuwakilisha chama na mgombea wake kituoni.

Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo la Kinondoni (DED) ambaye pia ni kada wa CCM hadi jioni ya leo alikuwa amegoma kutoa viapo kwa mawakala wa CHADEMA na vyama vingine huku wale wa CCM wakiwa walishapewa.

Kukosa viapo kuna maana wakala hatoruhusiwa kukanyaga kituoni na CCM wangelibakia wenyewe vituoni. Baada ya kufunga kampeni jioni ya leo, Mhe. Freeman Mbowe aliambatana na mawakala kwenda kwa msimamizi wa uchaguzi (ofisini).

Wakiwa njiani wakazingirwa na magari ya Polisi huku wakishambuliwa kwa risasi za moto na mabomu. Huwezi kuamini kama mambo haya yanatokea Tanzania! Mawakala kadhaa wa CHADEMA wamepigwa risasi za moto, wengine wamejeruhiwa kwa virungu, magongo n.k.

Katika upigaji huo wa risasi za MOTO tena hovyo hovyo, INASEMEKANA KUWA Polisi wamemuua mwanafunzi wa Mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM),Aqulina Akwilini Baftaha, ambaye amepigwa risasi akiwa kwenye daladala. Mwanafunzi huyu alikuwa safari yake na wala hakuwa kwenye mkutano wa Chadema. Risasi za Polisi wetu zimemfikia huko huko, na INAELEZWA KUWA hivi sasa ni marehemu.

Nimeumia sana! Nimejeruhiwa moyoni! Roho inaniuma mno. Kwa nini? Kwa nini tunapiga watu wasio na hatia risasi za moto? Nani ametoa amri hiyo? Ni kwa nini tunashambulia watu waliokuwa wanakwenda kudai viapo vyao kwa sababu saa 11 alfajiri wanapaswa kuwa vituoni?

Kwamba baada ya DED wa Kinondoni kuwanyima viapo, mlitaka wafanyeje? Kwa nini tunaifukuza amani? Kwa nini tunaua raia wasio na hatia? Kwa nini tunavamia na kuwapiga watu hata wasio na jiwe mkononi? Kwa nini tunatumia risasi za moto kuwapiga watu wetu?

Nchi yangu inaniuma sana. Mama Tanzania anateketea!

Huyu Mkurugenzi wa Kinondoni, ametoa viapo hivyo usiku huu, baada ya watu kupigwa risasi, kina John Heche (Mbunge wa Tarime) kukamatwa, mawakala wa CHADEMA kukamatwa na mwanafunzi aliyekuwa na safati zake kuuawa.

Huyu Mkurugenzi wa Kinondoni alitumwa na nani kutoa viapo baada ya watu kufa? Nadhani sasa CCM wamo shereheni, sherehe za damu! Hawawezi kutafuta madaraka bila kumwaga damu, bila kunywa damu! Madaraka ya damu, wanaoga damu, wanafungua kinywa kwa damu, wana-lunch damu na ku-dinner damu.

Damu!

#Mtatiro J
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad