“Ukicheza Simba, Yanga, Ukaondoka Wanasahau bado ni Mchezaji Mzuri”-Humud

Watu wengi wamekuwa wakitafsiri mchezaji aliyefanikiwa kucheza ligi kuu anaporudi ligi daraja la kwanza biashara yake inakuwa imekwisha, lakini kiungo mkongwe Abdulhalim Humud ‘Gaucho’ hakubaliani kabisa na jambo hilo na bado anaamini yuko fit kushindana na wachezaji wengine wa VPL.

“Mpira wa kibongo una mambo mengi hasa kwetu sisi wachezaji wazoefu ambao tumeshapita kwenye vilabu vikubwa, mpira wa tanzania ukishacheza simba na yanga ukiondoka watu wanasahau kwamba wewe bado ni mchezaji mzuri lakini vilabu hivyo vinahitaji kuwa na wachezaji wengine wapya hicho ndio wanasahau,” Abulhalim Humud.

“Kile ambacho kilinifanya nije kmc leo nimeweza kukitimiza pamoja na wachezaji wenzangu na tumeifikisha pale ambapo wanakinondoni wanataka iwepo.”

“Kizuri zaidi mpira ni mchezo wa hadharani sio kujificha kile ambacho kimefanyika au ambacho nakifanya tangu nimekuwa kmc kinatosha kuwa majibu kwa watu ambao walikuwa wanafikiria tofauti.”

Humud alifunga goli pekee lililoipandisha daraja KMC kwenye mchezo wa mwisho wa
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad