Umoja wa Ulaya Watoa Tamko Mauaji Utekaji Nchini

Umoja wa Ulaya Watoa Tamko Mauaji Utekaji Nchini
Umoja wa Ulaya (EU) umetoa tamko kuhusu matukio ya utekaji na mauaji yanayotokea nchini, ukiitaka Serikali kufanya uchunguzi wa kina.

Taarifa ya umoja huo uliyotolewa leo Februari 23, 2018 inaeleza kuwa imetolewa na ushirikiano wa mabalozi wa nchi wanachama wa umoja huo wenye uwakilishi Tanzania na kuungwa mkono na mwakilishi na mabalozi wa Norway, Canada na Uswisi.

“Tunashuhudia kwa wasiwasi mwendelezo wa matukio ya hivi karibuni yanayotishia nidhamu ya kidemokrasia na haki za Watanzania, katika nchi iliyojizolea umaarufu mkubwa duniani kwa utulivu, amani na uhuru.”

“Tumesikitishwa na kifo cha mwanafunzi aliyepigwa risasi mwisho wa juma lililopita Akwilina Akwilini, anayeombolezwa nchi nzima. Tunakaribisha wito wa Rais John Magufuli wa uchunguzi wa haraka,” inaeleza taarifa hiyo.

Katika taarifa hiyo EU imetoa wito wa uchunguzi wa kina kwa vifo vyote vya wanaharakati wa kisiasa na haki za binadamu.

“Tunatoa pole za dhati kwa familia zao zote. Tuna wasiwasi na ongezeko la ripoti za ukatili katika miezi ya hivi karibuni, kama vile, jaribio lililohatarisha maisha ya mbunge Tundu Lissu; kupotea kwa watu kama mwandishi wa habari Azory Gwanda na mashambulio yaliyopoteza uhai wa viongozi wa Serikali,” inaeleza EU.

Umoja huo umesema pia yametokea matukio yaliyowahusisha wawakilishi wa vyombo vya usalama na wananchi Mkoa wa Pwani ndani ya miaka miwili iliyopita.

“Tunaungana na Watanzania katika kuwaomba wahusika wote, kutunza amani na usalama wa michakato ya kidemokrasia, watu wake na kuheshimu utawala wa sheria bila udhalimu.”

Akwilina alipigwa risasi Februari 16,2018 eneo la Kinondoni Mkwajuni, wakati Polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakielekea ofisi za msimamizi wa uchaguzi wa ubunge Jimbo la Kinondoni kudai viapo vya mawakala wao.

Lissu ambaye ni mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) na Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), alipigwa risasi Septemba 7,2017 nje ya makazi yake mjini Dodoma. Kwa sasa yupo nchini Ubelgiji akiendelea na matibabu.

Azory ni mwandishi wa habari wa kujitegemea wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), aliyetoweka tangu Novemba 21, 2017 Leo ametimiza siku 95 tangu alipopotea.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Madai ya ukosefu wa utulivu Tanzania kutoka kwa jumuia za kimataifa ni matunda ya mikakati ya Chadema ya kulipaka matope Taifa kwa kisingizio cha mapambano ya kutafuta demokrasia. Hakuna tukio la vurugu la kisiasa linalotokea Tanzania lisilokuwa na mkono wa Chadema. Kama kauli mbiu kuu ni Tanzania kwanza kwanini kama watanzania tuendelee kukisapoti chama chenye malengo ya kuliangamiza taifa kwa maslahi ya chama na baadhi ya watu fulani na sio Taifa? Kwa asilimia mia moja 100% Chadema na washirika wake wanapinga na kubeza jitihada zozote za maendeleo zinachokuliwa na serikali na badala yake wameamua kusapoti mitandawazi ya kulisaliti taifa nje na ndani ya nchi . La kushangaza zaidi kwanini mamlaka husika inayohusika na usimamizi wa vyama vya siasa nchini wanalegalega kukichukulia Chadema hatua za kinidhamu ikiwemo hata kukifutia usajili wake kwani ni dhahiri Chadema inakoelekea ni kuja kusababisha maafa zaidi kwa Tanzania. Mfano zile vurugu walizoanzisha na kupelekea kifo cha mwanafunzi kwa watanzania wengi ni msiba lakini kwa Chadema na washirika wake ni jambo la faraja kubwa kwa wao kutokea wakati huu kwani utaona jinsi gani Chadema wanavyotumia kifo cha yule Mwanafunzi kama mtaji mkubwa wa siasa bila hata aibu. Kwa mtazamo wangu kwa taifa lolote duniani linapokuja suala la maslahi ya nchi hasa kuhusiana na masuala ya usalama huwa hakuna cha kumuonea mtu au taasisi yeyote muhali. Ndio maana Wamerekani zaidi ya laki tatu na zaidi waliuwana wenyewe kwa wenyewe kuhakikisha Marekani inakuwa moja na hiyo yote ilikuwa ni katika jitihada zao za kulinda maslahi yao ya kwanza kuliko ya baadhi ya watu fulani. Ukienda China utakutana na habari hizo hizo za kutokuwa na huruma na taasisi yeyote ile yenye nia ya kuhatarisha maslahi ya Taifa lao hasa katika masuala ya usalama . Kule Misri kila mtu anafahamu nini kilitokea na sio kama nasapoti kilichotokea hadi kupelekea raisi mteule na serikali yake halali kufurushwa na baadhi ya viongozi wake kusekwa jela hadi hivi tunavyozungumza labda yaliyotokea Misri yalilenga kuangalia maslahi ya nchi zaidi kuliko ya chama fulani. Sasa kama mtanzania najiuliza kwa nini Chadema wanaachiwa kuendeleza harakati za kulidestroy Taifa kwa maslahi ya nani? Au mpaka watakapokuja kusababisha maafa makubwa zaidi ndipo tutakapokujaamka na kuanza kujuta. Kwa wale wanoishabikia Chadema na kuzani yakuwa itakuja kuwa na tija na Taifa waachane kabisa na ndoto hizo kwani siku zote vitu huenda kwa mifano kabla ya kuwa vitu halisi. Mbowe amekuwa mwenyekiti wa maisha pale Chadema. Lema amekuwa mropokwaji na mtu wa kuhamasisha vurugu. Na baadhi ya viongozi wake wengine wamekuwa msitari wa mbele kuhamasisha wafuasi wao juu ya uvunjifu wa amani sasa niambie viongozi wa namna hiyo waje wakabidhiwe nchi hilo Taifa litakuwa la namna gani?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad