Uongozi Waifungia Baa Aliyekuwepo ‘Mowzey Radio' na Kujeruhiwa

Uongozi Waifungia Baa Aliyekuwepo ‘Mowzey Radio' na Kujeruhiwa Yafungwa
Uongozi wa Jiji la Entebbe nchini Uganda umeifunga  Baa  ya De ambayo mwanamuziki Moses Ssekibogo maarufu kwa jina ‘Mowzey Radio’ alikuwapo na kujeruhiwa wiki mbili zilizopita.

Mwanamuziki huyo alifariki dunia jana katika Hospitali ya Case alipokuwa akipatiwa matibabu.

Gazeti la Daily Monitor nchini humo limeripoti kuwa agizo la kufungwa kwa baa hiyo limetoka kwa Meya wa Jiji, Paul Kayanjana.

 Mbali na kuchukua hatua hiyo, Meya Kayanjana ameagiza apelekewe vibali vyote  vya baa  hiyo  ikiwamo leseni na  kuwekwa  makufuli  katika milango yote.

Hata hivyo, ameonya kuwa endapo mmiliki wa baa hiyo atakaidi amri  hiyo ya kutoendelea na uendeshaji atatozwa faini ya Sh1milioni  za Uganda ambazo atapaswa kuzilipia kupitia Benki  ya Stanbic, Tawi la Entebbe.

Katika hatua nyingine, watu wameonekana kuzidi kumiminika katika ukumbi wa  Taifa wa maonyesho ambako wananchi watauaga mwili kabla ya maziko yatakayofanyika kesho saa 10 jioni Kaga, Barabara ya Entebbe.

Mwanamuziki Radio aliyewahi kutamba na kundi la Goodlyfe alilazwa katika Hospitali ya Case baada ya kushambuliwa katika ugomvi uliotokea wiki mbili zilizopita katika Baa ya De.



Ugomvi huo unaodaiwa kuwa kati yake na mlinzi wa baa hiyo, ulimsababishia apasuke fuvu na kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kwa wiki mbili.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad