Ushirikiano mpya kati ya Tanzania na Kenya ni pigo jingine kwa Upinzani


Siku za hivi karibuni wapinzani nchini mwetu walizigawa siasa za Kenya katika wings mbili za Team CCM na Team UKAWA. Mara zote walichukulia kama NASA wapo upande wa CCM wakati JUBILEE wakichukuliwa kama ni team UKAWA. Katika hali hiyo chochote kilichokuwa kikifanywa na Rais Uhuru Kenyatta wenzetu hawa walikitumia kama case study katika kuiponda serikali ya Tanzania na hata mara nyingine kuonekana kupandikiza chuki za dhahiri kabisa kati ya serikali hizi mbili; ya Tanzania na ile ya Kenya.

Sasa uamuzi wa Marais hawa wawili Magufuli na Kenyatta, kushirikiana katika nyanja mbalimbali; na wao ku-declare wazi kabisa kwamba hawana ugomvi au tofauti nyingine kati yao waweza kuwa ni pigo kwa upinzani ambao muda wote wamekuwa wakihubiri kuwepo kwa hali ya kutoleewana kati ya Marais wa nchi hizi mbili. Ni pigo kwao kwa sababu walijipambanua wazi kabisa kama UKAWA Alliance (na si mtu binafsi) kuwa wako attached na Jubilee Alliance na mara nyingi walionekana wakihudhuria kwenye shughuli za kisiasa za umoja huo.

Tusishangae kuona wenzetu hawa wanabadilika na kuanza kuponda pale nchi hizi mbili zitakapoingia katika makubaliano ya mambo fulani, ambayo kabla walikuwa wakiyatumia kama bakora ya kuichapa serikali ya Tanzania. Tusishangae kuona Kenyatta anakuwa adui yao na wao kutomtumia tena kama Rais wa kumtolea mifano kama walivyokuwa wakifanya awali kisa tu kwamba yupo karibu Rais Magufuli.

Ni vema sasa upinzani wakaupongeza kwa dhati ushirikiano huo, kwani ni dhahiri utakuwa katika mambo ambayo wamekuwa wakiyatolea mifano hapo awali.

By MwanaPekee
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad