Vanessa Mdee: Mimi na Diamond ndio tunaosikika Nigeria


Msanii wa muziki Bongo, Vanessa Mdee amesema muziki wa Afrika Mashariki haupewi nafasi kubwa nchini Nigeria kama inavyokuwa ikitazamiwa.

Muimbaji huyo ambaye yupo nchini humo kwa ajili ya kutangaza albamu yake ‘Money Mondays’ ameiambia Clouds Fm kuwa katika moja club alizopita alikuta ngoma zinazochezwa ni ya Patoranking na Diamond ‘Love You Die’ na ile aliyoshirikiana na Reekado ‘Move’.

“Hapa Nigeria haupo kabisa muziki wa Tanzania, haupo kwa nguvu ambayo unatakiwa kuwepo kwa sababu tunaelewa muziki wetu ni mkali, wasaniii wetu ni wakali. Kidogo wanauzito wa kupokea muziki wa East Africa, jana nilikuwa club nilisikia nyimbo za Tanzania ambazo zinapigwa ni ile Diamond na Patoranking na ya kwangu  na Reekado ‘Move’ hakuna nyimbo nyingine inapigwa hata ya Afrika Mashariki,” amesema.

Pia Vanessa amesema si kwamba hawatambui muziki kutoka Afrika Mashariki ni mzuri ila wameamua kuupa kipaumbele muziki wao na kutokana na idadi kuwa wasanii walionao inakuwa ni vigumu kwa muziki kutoka sehemu nyingine kupata nafasi.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ukisema eti wewe na Diamond ndio mnasikika Nigeria kivipi? sikweli. Ningekubali kama wanasikiliza ngoma zako na Diamond bila kushirikiana na Mnageria. Sasa hizo mlizo shirikiana nao ndo wanasikiliza kwa sababu kuna mnageria ndani alafu unasem eti wewe na Diamond ndio mnasikika kivipi kwa ngoma gani yako ao Diamond bila Mnageria.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad