Baadhi ya viongozi saba wa Chadema wanaelekea Kituo Kikuu cha Polisi kuitikia wito wa kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa.
Akizungumza na MCL Digital leo Februari 20, 2018 mkurugenzi wa itifaki, mawasiliano na mambo ya nje wa Chadema, John Mrema amesema viongozi hao wanajiandaa muda huu kuelekea kituoni.
Viongozi walioitwa na Mambosasa ni mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, katibu mkuu wa chama hicho, Dk Vincent Mashinji, manaibu katibu wakuu (bara), John Mnyika na Salum Mwalimu (Zanzibar).
Pia wamo, mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima Mdee; mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti, John Heche na Ester Matiko ambaye ni mweka hazina wa Bawacha.
Jana, Mambosasa aliieleza MCL Digital kuwa viongozi hao ni watuhumiwa na kama wameitwa polisi ni fadhila tu, ila kwa yaliyotokea wanapaswa kukamatwa.
Wito wa viongozi hao polisi umekuja siku siku nne tangu kutokea kwa kifo cha Akwilina Akwiline, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo cha Taifa cha Usfairishaji (NIT).
Akwilina aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya daladala eneo la Mkwajuni, Kinondoni jijini Dar es Salaam wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakienda ofisi za mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni kudai viapo vya mawakala wao.
Hili ni Jambo la kusababisha umwagaji Damu ya Mtoto asiekuwa na Hatia.
ReplyDeleteHawa na kiongozi wa Genge hili lao wote ni wa kuweka ndani kwa mujibu wa sheria na Kesi yao haraka
baada ya Upelelezi kukamilika ni kutoka ndani na kupelekwa kujibu shtaka stahiki la Usababishaji umwagaji wa Damu katika kulinda Amani na utulivu ambao wao ndiyo shinikizo halisi wa tukio.
Mambosasa... Tunakuamini na AG na DPP tunaimani nanyi katika kumtendea haki Damu mbichi ya mtoto wetu mwana chuo ambae lilikuwa moja ya tegemeo la Taifa na Familia yake kuendeleza na kulitumikia Taifa letu la Tanzania.
Sheria iko wazi... na vielelezo na viashiria pia viko wazi.
Nia za hawa waleta Tafaruki na Lengo la kuvunja utulivu na Amani.. wana Historia Nalo.
Tutawazibiti na kuwaweka mahali stahiki... Tanzania yetu ni ya Salama na Amani. Na tutaendelea kuwa nao.. Wachache hawa hawana nafasi katika Usalama wetu na mila zetu na desturi zetu hapa Tanzania.
mungu amlaze pema panapostahiki Marehemu na kuwapa utulivu na ujasiri wafiwa na Familia yake na wote wakaribu waliguswa na Kifo Hichi. Ameen.
Mambosasa .... Jukumu unalo na wote waliopo katika mlolongo wa Usalama na Amani katrika nchi yetu.