Ikiwa ni kipindi cha maadhimisho ya miaka 41 ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi ccm, viongozi wa chaa hicho wilayani Bagamoyo wamelalamika juu ya kutoridhishwa na utendaji kazi wa mkurugenzi wa halmashauri ya Chalinze na kwamba amekua kikwazo katika kuharakisha miradi ya maendeleo.
Akitoa malalamiko hayo mbele ya mwenyekiti wa Ccm wilaya ya bagamoyo ndugu Abdulzahoro Rashid katika sherehe za maadhimisho ya miaka 41 ya ccm zilizofanika katika ukumbi wa shule ya sekondari Lugoba, diwani wa kata ya Lugoba bi Rehema Mwene amesema kumekua na hali ya sintofahamu kwenye mradi wa upanuzi wa kituo cha afya Lugoba uliotengewa shilingi milioni 400 ambazo zilitakiwa kutumika tangu mwezi januari redha ambazo mpaka sasa haijafahamika nini kimekwamisha .
"Nimejitahidi kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji cha lunga kuwahamasisha waanchi kujitolea kusafisha eneo la ujenzi huo na tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa sambamba na kushiriki kuchimba msingi lakini cha ajabu fedha ambazo zilishaletwa halmashauri bado hazifahamiki nini kimekwamisha kufika mahali husika" alisema diwani huyo
Mradi huo ambao umelenga kuongeza majengo ya Wodi ya mama na mtoto, nyumba ya mganga wa kituo, chumba cha kuhifadhia miili ya marehemu, Wodi ya wazazi pamoja na wodi ya watoto
Kwa upande wake mwenyekiti wa Ccm wilaya ya Bagamoyo ndugu Abdulzahoro Rashid amesema vitendo vya kuchelewesha miradi ya maeneleo sio vya kufumbia macho na yeye kama msimamizi wa ilani ya chama atahakikisha anakutana na mkurugenzi huyo kujua sababu za kuchelewa kwa kuanza kwa ujenzi huo lakini pia atamtaka mkurugenzi huyo kujitathmini juu ya malalamiko mengi yanayomkabili kutoka kwa viongozi na wananchi wa chalinze juu ya utendaji wake na ikibidi aombe kujiuzuru
"kuna haja gani ya kuendelea kumnyamazia kiongozi anayerudisha nyuma jitihada za Mh rais Magufuli kwa kuchelewesha miradi ya maendeleo kwa kweli hili ni bomu " alisema ndugu Zahoro
Aidha kwa upande mwingine mwenyekiti huyo ametangaza kuunda kamati maalum itakayohusika na kukagua mali zote za chama pamoja na kupitia mikataba yote iliyosainiwa na viongozi wasio wazalendo na atakayebainika atafikishwa katika mikono ya sheria
"chama kimekua kama shamba la bibi kila mtu anachuma na kujinufaisha mwenyewe, kuna watu tangu mwaka 2000 mpaka leo mikataba yao haijaisha na wanaangaliwa tu" aliongeza mwenyekiti ndugu Zahoro
Kamati hiyo inaongozwana mwenyekiti ndugu yahya Msonde pamoja na katibu wake ndugu boubakar Mlawa huku wajumbe wa kamati hiyo wakiwa ni Bolizozo (Mwenezi wa wilaya), Mkwayu Makota (M/kiti Uvccm), Latifa Kizota ambao mpaka sasa tayari wameanza kazi hiyo na wanaendelea na uchunguzi na baada ya siku 10 wanatarajia kukabidhi ripoti kwa mwenyekiti