Viongozi wa CHADEMA wakiongozwa na Mbowe, waenda NEC kuwasilisha malalamiko kuhusu Uchaguzi ubunge Jimbo la Kinondoni

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe, mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kupitia chama hicho Salum Mwalimu na baadhi ya wabunge wa chama hicho, muda huu wapo ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Wakitaka kuonana na Mkurugenzi wa tume hiyo.

Lengo la kuwasilisha malalamiko yao kuhusu mchakato wa uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Kinondoni Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa NEC hawajamkuta, ila wameweza kuongea kwa simu kwa kutumia simu ya mmoja wa Maofisa wa NEC baada ya kutopokea simu ya Mbowe. Wamekubaliana kwamba Malalamiko yote waliyo yawasilisha yatatatuliwa leo hadi kufikia jioni.

 Mwenyekiti wa Taifa wa (Chadema) Mhe Freeman Mbowe na viongozi wengine wa chama hicho wamekwenda ofisi ya NEC, kushinikiza wapewe viapo vya mawakala wao ambavyo mpaka sasa hawajapewa huku wakidai mawakala wa CCM wameshapewa.

Msafara huo wa viongozi hao ulipofika ofisi hizo kwa lengo la kukutana na Mkurugenzi wa Tume hiyo, Ramadhan Kairima waligonga mwamba baada ya watumishi wa NEC kudai kuwa Mkurugenzi huyo hayupo ofisini, viongozi hao waligoma kuondoka katika ofisi hiyo mpaka baadae Mbowe aliongea kwa simu na Mkurugenzi huyo na kukubaliana.

Zifuatazao zilikuwa kauli za viongozi hao wakiwa kwenye ofisi hiyo ya NEC
Mbunge wa Kawe Mhe Halima Mdee "Mnadhani tumekuja kunywa soda hapa sisi tumeacha shughuli muhimu kuliko hata nyinyi mnaokula ugali hapa, wewe tuma mtu aende pale amcheki Mkurugenzi ilo ndiyo jambo la mbolea ila hapa hatutoki, piga simu mtume mtu aulize kama Mkurugenzi yuko pale tunagawa timu wengine wanakwenda wengine tunabaki hapa"

Kwa upande wa Mhe John Heche alikuwa na haya ya kusema "Kailima huyu kwenye Uchaguzi Mkuu nimempigia simu huyu madiwani wameondolewa nje ya utaratibu akarudisha leo kuongea na sisi moja kwa moja anashindwa nini? Na simu hapokei pia hata tulikuwa hatuna haja ya kuja hapa tunapiga simu hapokei, sisi tunamkutano jioni turuhusu tuingie tuonane naye twende kwenye mkutano, nyinyi mshaanza kusema tumevamia ofisi zenu kwa nguvu"

Mbali na huyo Mbunge wa Bunda mjini Mhe Ester Bulaya naye alifunguka na kusema kuwa tayari mawakala wa Chama Cha Mapinduzi "CCM viapo wameshapewa wengine hamtaki kuwapa kama mnawaogopa watu mnaowagopa wa nini, sisi tusishiriki uchaguzi nyinyi mtapata faida gani"

Aidha Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa naye alihoji "Au ndugu zetu mmeshapanga kutangaza matokeo mnavyotaka nyinyi"

Baada ya vuta vutana hiyo ya maneno baadaye Mhe Mbowe aliweza kuingia ndani na alipotoka alikuwa na haya ya kusema kwa viongozi wengine wa Chadema waliofika hapo

"Nimemwambia kwamba sisi tumekuja kwa sababu hapokei simu zetu na maandishi yetu hayajibiwa kwa wakati na uchaguzi umekaribia na kuna mambo chungu nzima ya kurekebishwa kabla ya uchaguzi kwa hiyo tumekubaliana kwamba yeye naye lazima aitishe kikao chake na Tume ya Uchaguzi tukubaliane nao malalamiko gani ambayo tunayo halafu tupate muafaka kisha baadaye mchana awe amefanya mawasiliano, kama tutakutana tena mchana kuelekea jioni ili ratiba zingine ziendelee kwa hiyo mimi nimeridhika na hilo sioni kama kuna tatizo kwa hiyo cha msingi Waheshimu ninataka watu watatu wanne tukae sehemu tujadili mambo yetu halafu tumpigie simu maana anasubiri simu yetu jambo hilo" alisema Mhe Mbowe. VIDEO:
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad