Waandamanaji Waweka Kambi Nje ya Ikulu ya Marekani Wakishinikiza Kubadilishwa kwa Sheria ya Bunduki

Waandamanaji Waweka Kambi Nje ya Ikulu ya Marekani Wakishinikiza Kubadilishwa kwa Sheria ya Bunduki
Vijana wengi na familia zao Jumatatu waliwasilisha kwenye Ikulu ya White House hoja yao ya kutaka sheria kali ya kudhibiti silaha ikiwa ni chini ya wiki moja baada ya mtu mmoja mwenye bunduki kuwashambulia wanafunzi na kusababisha vifo vya watu 17 katika jimbo la Marekani la Florida.

Watu wapatao 50 waliandamana Washington DC wakiwa na mabango yaliyoandikwa “Imetosha” na “Badili sheria za bunduki au badili Congress”.

Mkusanyiko huo umekuja katikati ya harakati zinazoongezeka za kutoa wito kwa Rais Donald Trump na wabunge wengine kuimarisha sheria za umiliki wa bunduki za Marekani wiki moja baada ya kufanyika shambulio baya dhidi ya wanafunzi katika historia ya nchi.

Watu wapatao 17 waliuawa pale mtu mmoja aliyekuwa amejihami kwa bunduki alipofyatua risasi kuwashambulia wanafunzi na walimu katika Shule ya Sekondari ya Marjory Stoneman Douglas Jumatano iliyopita.

Katika maandamano hayo ya Washington, waandamanaji walikuwa wakisoma majina ya waliouawa katika shambulio hilo lililofanyika Marekani kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1999.

"Wako hapa kwa sababu wanasema sasa inatosha wakati umefika kwamba watoto shuleni wanapaswa kulindwa na ikiwa hiyo itamaanisha kubadilisha sheria za umiliki wa bunduki, basi hicho ndicho kinapaswa kutokea," alisema Fisher.

Trump pamoja na maofisa wengine wako chini ya shinikizo la kuacha ushirikiano na Chama cha Taifa cha Bunduki (NRA), kikundi chenye nguvu cha kushawishi umiliki wa bunduki ambacho kimelalamikiwa kuwa sababu ya wabunge wa Marekani kusita kupitisha sheria ya udhibiti silaha.

"NRA: Acha kuua watoto wetu!" lilisomeka moja ya mabango ya waandamanaji Jumatatu.

Japokuwa rais alituma salamu za rambirambi kwa ndugu wa wafiwa kutokana na shambulio la Florida, kwa kiasi kikubwa amejizuia kuzungumzia mabadiliko ya sheria ya umiliki wa bunduki.



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad