Wahamiaji haramu wabuni njia mpya kuingia barani Ulaya
0
February 18, 2018
Wahamiaji haramu wagundua njia mpya ya kuingia katika mataifa ya Ulaya Magharibi kwa kupitia nchini Bosnia Herzegovina.
Hapo awali wahamiaji walikuwa wakipitia nchini Ugiriki, Makedonia, Serbia, Hungary au Kroasia kuingia katika mataifa ya Ulaya Magharibi.
Njia hiyo ambayo ilikuwa ikitumiwa na wakimbizi ilifungwa Machi mwaka 2016.
Kwa sasa wahamiaji haramu na wakimbizi wanajaribu kutumia Kroasia kupitia Bosnia Herzegovina kuingia katika mataifa ya Ulaya Magharibi kutafuta hifadhi.
Katika kipindi hiki cha baridi, maimamu katika hutoa hifadhi za muda kwa wahamiaji wanaoathirika na baridi katika safari zao.
Wahamiaji 35 wamepewa hifadhi na maimamu mjini Sarayevo wajikinge na baridi.
Wengi miongoni mwa wahamiaji hao ni raia kutoka Pakistan, Afghanistan, Syria, Libya na Morocco.
Jeshi la Polisi Bosnia limefahamisha kuwa watu zaidi ya 750 wameingia nchini humo kinyume cha sheria Januari mwaka 2018 wakitaraji kuendelea na safari yao Ulaya Magharibi.
Tags