Wakili Ataka Kortini Kuelezwa Maendeleo Kesi Mke wa Bilionea Msuya

Wakili Ataka Kortini Kuelezwa Maendeleo Kesi Mke wa Bilionea Msuya
Wakili wa utetezi, Peter Kibatala, ameutaka upande wa mashtaka katika kesi ya mauaji inayomkabili mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita (41), kuieleza mahakama hatua waliyofikia kuhusiana na upelelezi wa shauri hilo.

Mbali na Mriti, mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni mfanyabiashara, Revocatus Muyela (40) ambao wote wanakabiliwa na shtaka mmoja la mauaji ya dada yake bilionea Msuya, Aneth Msuya.

Kibatala alidai hayo jana mbele ya hakimu mkazi mkuu, Thomas Simba baada ya wakili wa Serikali, Patrick Mwita kudai kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi unaendelea.

Awali, wakili Mwita alidai mahakamani hapo kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika, hivyo anaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa na kufuatilia jalada kama limeshatoka kwa mkurugenzi wa mashtaka nchini (DPP).

Kutokana na maelezo ya pande zote, hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 21, huku akiutaka upande wa mashtaka watakapokuja kueleza hatua waliyofikia katika kesi hiyo.

Washtakiwa kwa pamoja wanakabiliwa na shtaka moja la mauaji, wanadaiwa kumuua Aneth.

Hata hivyo, Februari 23, 2017 washtakiwa hao waliachiwa huru na mahakama hiyo mbele ya hakimu mkazi mkuu, Godfrey Mwambapa kisha wakakamatwa tena na baadaye kusomewa shtaka moja la mauaji upya.

Katika kesi hiyo namba 5/2017, wanadaiwa kumuua kwa makusudi Aneth tukio linalodaiwa kutokea Mei 25, 2016 maeneo ya Kibada Kigamboni Jijini Dar es Salaam
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad