Wakuu wa Shule Binfsi Waonywa Ulipaji Ada

Wakuu wa Shule Binfsi Waonywa Ulipaji Ada
Wakuu wa shule binafsi mkoani Dar es Salaam wametakiwa kujitafakari mara mbili kabla ya kuwafukuza shule wanafunzi wanaoshindwa kulipa ada kwa wakati.

Rai hiyo imetolewa jana Februari 2, 2018 na ofisa elimu taaluma mkoani humo, Janeth Nsunza katika mkutano wa wakuu wa shule zote Dar es Salaam.

Nsunza amesema baadhi ya wamiliki na wakuu wa shule wanashindwa kuwavumilia wazazi wanapokwama kiuchumi na kushindwa kulipa ada za watoto wao kwa wakati.

Amesema baadhi ya wazazi wanaposhindwa kulipa ada hutakiwa na shule husika kula kiapo mahakamani.

“Kama mzazi ni mlipaji mzuri wa ada ikifika mahali  amekwama ni vyema viongozi husika wamwelewe na kumvumilia, wawe pamoja kwa raha na shida,” amesema,

“Kuna mzazi alifika ofisini kwetu  mwanae alikuwa kidato cha nne mwaka jana, hakuwa na ada akafukuzwa, lakini  akaandika barua kwa Kamishina wa elimu kuomba aruhusiwe kufanya mtihani huo.  Miongoni mwa nyaraka alizonionesha ilikuwepo  ya kuapa mahakamani.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad