Walioshuhudia walisema kuwa wanamgambo hao waliokuwa na magari waliwasili kwenye mji wa Dapchi, jimbo la Yobe siku ya Jumatatu, ambapo walianza kufyatua risasi na kulipua vilipuzi.
Mwezi Aprili mwaka 2014, Boko Haram waliwateka nyara wasichana wa shule 270 katika mji wa kaskazini mashariki wa Chibok.
Wakaazi na raia waliojihami huko Dapchi wanasema wanaamini wanamgambo hao walikuwa na mpango wa kuwateka nyara wasichana.
Wanasema kuwa vikosi vya jeshi la Nigeria vikisaidiwa na ndege za jeshi, baadaye vilizima shambulizi hilo.
Mwezi Septemba mwaka uliopita zaidi ya wasichana wa shule 100 wa shule ya Chibok waliunganishwa na familia zao kwenye sherehe katika mji mkuu wa Nigeria Abuja.
Sehemu kubwa ya wasichana hao waliokolewa mwezi Mei kufuatia mpango uliokumbwa na utata wa kubadilishana wafungwa na serikali ambapo makamanda wa Boko Haram waliachiliwa.
Lakini zaidi wa wasichana 100 bado wanashikiliwa na Boko Haram na haijulikani waliko.
Wanamgambo wa Boko Haram wamekuwa wakiendesha harakati za kutaka kuwa na taifa lao la kiislamu kaskazini mwa Nigeria. Mzozo huo unaaminiwa kusababisha vifo vya maelfu ya watu.