Wastara Aanza Matibabu India ..Atoa Ushahidi wa Picha Kuwakata Kidomo Waliokuwa Wanasema Anajifanya Kuumwa

Msanii huyo maarufu amekuwa akisumbuliwa na mguu wake huo ambao ulipelekea kufanyiwa upasuaji na kupewa mguu wa bandia licha ya hali yake kubadiilika hivi karibuni na kudai kuwa amekuwa akipata maumivu makali ambapo baada ya kupata matibabu ya awalialishauriwa kwenda nchini India kwa matibabu zaidi.

Akizungumza na mtandao wa Global Publishers Wastara amewashukuru Watanzania kwa michango yao kufanikisha matibabu yake.



“Nawashukuru Watanzania wote waliojitoa kunichangia ili niweze kupata matibabu, Namshukuru Rais Magufuli na mkewe Mama Janeth, peke yangu nisingeweza. Tulisafiri salama, tunamshukuru Mungu tumefika salama, kwa sasa nimeanza matibabu katika Hospitali ya Saifee hapa India.



“Kiafya nashukuru kwa kweli, najiskia vizuri kiasi japo bado mapema kuzungumzia maendeleo ya afya yangu kwa ujulma, lakini nawaombeni muendelee kuniombea kwa Mungu ili nipone, nirudi nyumbani salama,” amesema Wastara.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad